Na Dixon Busagaga,Hai
Wanandoa wawili wameuawa kinyama baada ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yusuf Njau
(32), anayeaminika kuwa ni mtoto wa kumzaa wa wanandoa hao, kuwakata kata kwa shoka
kisha kuchoma moto nyumba yao na kutokomea kusiko
julikana.
Tukio
hilo la kusikitisha na la aina yake limetokea juzi majira ya saa 12:30 jioni
katika kijiji cha Masama-Roo, kata ya
Machame Mashariki,wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro baada ya kijana huyo
kuchukua uamuzi huo kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Waliouawa
wametambulika kwa majina ya Shahidu Njau(60) ambaye ni baba yake mzazi na Minae Swai (57) ambaye ni mama mzazi wa mtoto
huyo.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho, Halfani Swai, alisema walipofika katika eneo la tukio baada ya
kusikia mayowe walikuta watu wakizima moto huku mwili wa mama mtuhumiwa ukiwa
umelala chini.
Alisema
wakati kijana huyo akiendelea kutenda unyama huo,alitokea baba yake mzazi, mzee
Shaidu aliyekuja kuingilia kati ugomvi
wa mama na mwanae lakini naye alikatwa kichwani kwa shoka.
Alisema
mwili wa baba ulikutwa ukiwa pembeni wa mwili wa mkewe ukiwa na majeraha ya
shoka kichwani.
Alisema
walimchukua kwa nia ya kuokoa uhai wake lakini muda mfupi baada ya kutoka
kwenye eneo la tukio wakiwa katika kituo cha mafuta maeneo ya Sadala Shaidu,
alipoteza maisha.
Taarifa
kutoka kijiji hicho zinasema muuaji, Yusuf Njau, ambaye amewahi kujifunza ngumi
akiwa Dar es Salaam pia aliwahi kuwatishia uhai baadhi ya ndugu zake zaidi ya
mara mbili.
Akizungumzia
hali hiyo, Mwenyekiti wa kijiji hicho, Halfani Swai, alisema kijana huyo ambaye
ni mkorofi pia aliwahi kutishia kuwaua shangazi na baba mdogo.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema
mtuhumiwa anatafutwa.
Alisema
miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Hai.
Kwa
upande mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga, alisema tukio hilo ni la kinyama na kuwataka wananchi kuwa
na subira huku akitahadharisha raia kutochukua hatua mikononi.
No comments:
Post a Comment