Na.Othman Khamis Ame
Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imekusudia kuongeza nguvu za ziada
katika kusaidia kuimarisha miundo mbinu ndani ya Bara la Afrika kwa lengo la
kuyajengea uwezo wa uzalishaji wa kiuchumi Mataifa mbali mbali yaliyomo
ndani ya Bara hilo .
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa China Bwana
Li Yuanchao wakati yeye na ujumbe wake alipofanya mazungumzo Rasmi na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza Ujumbe wa Zanzibar kwa
Niaba ya Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Bararaza la Mapinduzi Dr. Ali Moh’d
Shein hapo hoteli ya La gema Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Bwana Li Yanchao akiwa Zanzibar
kwa siku moja akiendelea na ziara yake ya siku sita Nchini Tanzania alisema katika utekelezaji wa azma hiyo
China
imejipangia kutumia Yuan Bilioni 2.2 katika mipango yake ya kuimarisha
miundo mbinu hiyo ya uwekezaji kwenye sekta ya biashara.
Aliishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuitumia fursa hiyo adhimu kwa kuchagua miradi
yake itakayoipa kipaumbele cha kwanza kwa kuwasiliana na Ofisi ya Ubalozi mdogo
wa Nchi hiyo uliopo Zanzibar
ili kuratibu miradi hiyo na hatimae hatua za utekelezaji zianze mara moja.
Bwana Li Yuachao alifahamisha kwamba China kupitia wataalamu wake itaangalia mfumo wa
uwekezaji uliopo hapa nchini na kuwashawishi wafanya biashara wa nchi hiyo
iliyopiga hatua kubwa kiuchumi kuwekeza miradi yao
katika visiwa vya Zanzibar .
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China
alipongeza uhusiano wa muda mrefu uliopo kati yaJamuhuri ya Watu wa China na
Tanzania na Zanzibar kwa ujumla na unastahiki uimarishwe zaidi kwa ustawi wa
baadaye wa pande zote mbili.
Alisema miaka mingi iliyopita ya
ushirikiano wa kindugu uliofikiwa kati ya pande hizo mbili imeipa faraja kubwa Tanzania kutokana na nguvu kubwa iliyopata ya
uimarishaji wa uchumi kupitia misaada mbali mbali inayotolewa na China .
“ Tumeshuhudia ziara za Viongozi wetu wakuu wa
pande zote mbili jinsi wanavyotembeleana ikionyesha wazi uthibitisho wa
uhusiano huo mkubwa unaopaswa kulindwa kwa nguvu zote “ . Alisema Bwana Li
Yanchao.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi akitoa shukrani zake alisema Zanzibar itaendelea kuiheshimu na
kuithamini China kutokana na msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar
katika harakati za kuimarisha uchumi.
Balozi Seif alieleza kwamba Jamuhuri ya Watu
wa China inastahiki
kupongezwa kwa misaada yake mikubwa inayotoa kwa Zanzibar
ambayo haijawahi kutokea katika Historia ya Zanzibar tokea Mapinduzi ya Mwaka 1964.
Alisema Wananchi wa Zanzibar
wamekuwa wakishuhudia misaada tofauti inayotolewa na China ndani ya kipindi cha miaka 50
tokea Mapinduzi iliyolenga katika sekta za afya, elimu, maji, miundo mbinu,
kilimo pamoja na mawasiliano.
Balozi Seif alieleza kwamba ujenzi wa maegesho
ya ndege katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, uwepo wa Madaktari wa Kichina
wanaofanyakazi katika hospitali mbali mbali nchini, ujenzi wa hospitali ya
Abdulla Mzee Mkoani Pembapamoja na ujenzi wa skuli ya Sekondari za Wilaya ni ushahidi
wa misaada hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliueleza ujumbe huo wa China
unaoongozwa na Makamu wa Rais wake kwamba wawekezaji wa nchi hiyo wako huru
kuitumia fursa iliyotolewa na Zanzibar
katika uwekezaji vitega uchumi ndani ya sekta ya Utalii.
Balozi Seif alisema Zanzibar
inahitaji kuwa na ukumbi mkubwa wa kimataifa utakaoweza kutoa huduma za
mikutano ya kimataifa sambamba na watalii wa China
kuombwa kupanga safari za kuitembelea Zanzibar .
Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais wa
Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Li Yanchao alifuatana na Mshauri wa Waziri wa
Mambo ya Nje wa China Bwana Qian Hongshan, Naibu Waziri wa Taasisi ya
IDCC ya Chama cha Kikoministi cha China Bwana Yu Hongjuu, Katibu Mkuu wa Vijana
wa Chama cha Kikoministi cha China Bwana Qin Yizhi, Balozi Mdogo wa China Bwana
Lu Yunliang pamoja na Naibu Waziri wa Fedha wa China Bwana Li
Junzao.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif katika mazungumzo hayo aliambatana na Balozi wa Tanzania
Nchini China
Balozi Abdullrahman Shimbo. Waziri wa Fedha Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee
pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dr.
Mwinyihaji Makame.
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofiri ya Rais
Utawala bora wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kepteni George Mkuchika,
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui pamoja
na mshauri wa Rais wa Zanzibar Balozi Mohd Ramia.
No comments:
Post a Comment