Enzi zetu zilikuwa ni ubunifu wa kutegeneza vitu mbalimbali vya mchezo kama inavyoonekana hapa Watoto wa Kijiji cha Kengwi wakipaki gari zao katika eneo la Kituo cha Kilimu kilioko kijiji kwao.Tafauti na Watoto wa siku hizi michezo yao mingi ni ya uvunjaji wa maadili ya michezo ya watoto na kuingia katika michezomya kuigana majanga kwao.
INEC yawataka wananchi kutumia siku zilizobaki kuboresha taarifa zao
-
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imewataka wananchi wa mikoa 15
inayotekeleza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga K...
44 minutes ago
Mdau unayosema ni kweli, lakini tujiulize kwani watoto huiga au sisi wazee ndio tunaowaandalia mazingira ya kuiga??
ReplyDeleteAngalia mada ya chini hapo yenye maudhia Happy Birth day Sumaiya. 10yrs. Utaona kwamba wazee ndio waliowaandalia watoto wao wafuate mila na desturi zisifaa kabisa. Ukuliza hasa nini maana ya hizo kofia walizovaa/walizovalishwa unaweza kugundua zina maana mbaya kabisa kiasili ya huko tulikoiga, pengine hata kidini ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini yetu.
Si watoto bwana wa kulaumiwa, ni sisi wazee, watoto mara nyingi hufuata wanayoyaona, wanayoyasikia au wanayofanywa imma na wazee nyumbani au mitaani. Sijui tuanze wapi lakini kwa kweli wazee tuna jukumu kubwa kwa Allah kesho juu ya malezi bora ya watoto wetu. Kila mmoja miongoni mwetu ni mchunga na ataulizwa juu ya kile alichokichunga.