Na Fatina Mathias, Dodoma
DAWA ya asili ya Mchungaji Ambilikile
Mwasapila wa Loliondo mkoani Arusha
maarufu kama 'kikombe cha babu ' kilichoaminika kutibu ugonjwa wa Ukimwi na
magonjwa mengine sugu,hakikutibu na badala yake kiliua watu wengi zaidi
waliokuwa wameathirika na magonjwa mbali
mbali ukiwemo Ukimwi,bunge limeelezwa.
Akiuliza wali la nyongeza jana bungeni mjini
hapa,Mbunge wa Nzega, Khamis Kigwangala ( CCM) aliitaka serikali kueleza kama
hatua zozote zilichukuliwa baada ya dawa hiyo kutoonesha matunda yaliyokusudiwa
na badala yake kuua zaidi.
Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Afya,
Dk.Stephen Kebwe, alisema hakuna ushahidi wowote ulioonesha wagonjwa
waliokunywa kikombe cha babu walikufa kwa ajili hiyo.
Alisema kufuatia utafiti uliofanywa na kituo
cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ulionesha dawa hiyo haikuwa na
madhara kwa
matumizi ya binadamu na kusema
waliokufa,ilikuwa ni kutokana na magonjwa yaliyokuwa yakiwakabili.
Awali katika swali lake la msingi,Kigwangala
aliitaka serikali kuruhusu hospitali zote kutibu wagonjwa hao ili kila mmoja
atibiwe na daktari anayemtaka huku akisema kwa sasa wananchi wana uelewa kuhusiana
na ugonjwa huo na madaktari wengi wanauelewa
pia.
Pia alitaka kujua kwa nini dawa za kupunguza
makali ya ugonjwa huo (ARVs) hazipo kwenye hospitali zote hasa kwenye maduka ya
dawa.
Akijibu hilo, Dk. Kebwe alisema, hadi kufikia
Disemba 2013 ,hospitali zote na vituo vya afya na baadhi ya zahanati nchini
zilikuwa zinatoa huduma ya
matunzo na tiba ikijumuisha dawa za kupunguza
makali ya Virus vya Ukimwi kwa watu wanaosihi na VVU.
No comments:
Post a Comment