Habari za Punde

Mahafali ya 21 Kidatu cha Sita Skuli ya Sekondari Lumumba Zenj.

Wanafunzi wa Kidatu cha Sita Skuli ya Lumbu Unguja wakionesha mchezo wa kugombea mali wakati Mzazi akiwa amaumwa Ndugu na Jamaa hugombea mali.Wanafunzi hao wakiwa katika mahafali yao ya 21, ya kumaliza masomo ya Sekondari na kuendelea na Elimu ya Juu.
Wanafunzi waliomaliza masomo ya Kidatu cha Sita katika Skuli ya Lumumba wakiimba wimbo maalum baada ya onesho lao la kutowa mafunzo kwa baadhi ya Watu hugombea na kugawana mali wakati muhusika akiwa kitandani anauguwa.

Wanafunzi wa Kidatu cha Sita Skuli ya Lumumba ambao wamemaliza masomo yao ya Elimu ya Sokondari wakionesha maonesho ya Mavazi ya Mataifa mbalimbali wakati wa Mahafali yao ya 21 ya Skuli ya Sekondari ya Lumumba Zanzibar, 

            Wanafunzi walioshiriki maonesho ya mavazi wakiwa jukwaani baada ya kumalizo show yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.