Na Joseph Ngilisho,Arusha
SAKATA la msichana wa ndani mwenye umri
wa miaka 16,aliyedaiwa kuuliwa na mama mwenye nyumba, aliyetajwa kwa jina la
Valentina Maxmillan (37) mkazi wa en
Moromboo jijini hapa,limechukua sura mpya baada ya mume wa mwanamke huyo,John Mwacha,
kuibuka na kusema kwamba amemwachia Mungu suala hilo.
Taarifa za awali zinadai kwamba mke wa
mfanyabiashara huyo (Valentina) aliimuua
msichana wake wa ndani na kisha maiti yake kuipeleka usiku wa manane hospitali
ya mkoa Mount Meru,kisha wao kurejea nyumbani na kuendelea kuangalia mechi ya kombe la dunia kwenye televisheni.
Mmoja wa majirani katika eneo anakoishi
mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambaye aliomba jina lake kutojatwa gazetini, alisema mwanamke
huyo ambaye ni jirani yao amekuwa akimtesa msichana huyo kwa muda mrefu kwa
kumpiga,kunyonyoa nywele na wakati mwingine kumnyima hata chakula na kusababisha afya ya msichana
huyo kudhoofika.
Alisema siku ya tukio walisikia kelele na
mtu akilia huku kelele hizo zikiambatana na sauti ikisema ‘leo ndio mwisho
wako’,hata hivyo majira ya usiku wa manane mlinzi wa duka la vifaa vya ujenzi lililopo jirani na nyumba ya mtuhumiwa, aliona
gari ndogo zikija katika nyumba hiyo kisha mlango kufunguliwa.
Naye mlinzi huyo (jina linahifadhiwa),alisema
aliona gari mbili ndogo zenye rangi nyeupe zikija kwa nyakati tofauti.
“Gari ya kwanza ilifika na kukaa kwa muda
kama dakika kumi ikaondoka nahisi walishindwa kupatana gari hiyo
ikaondoka,baada ya dakika 20 ilikuja gari nyingine na baadae lango
lilifunguliwa,niliona kitu kama furushi likiwa limefunikwa nguo huku baba
mwenye nyumba ndiye aliyekuwa amebeba na kuweka kwenye gari,” alisema.
“Nilishangaa kusikia baadae asubuhi kuwa
kumbe lile furushi lilikuwa lina maiti ya huyo msichana,” alisema.
Hata hivyo, mlinzi huyo alisema yeye
binafsi hajui chanzo cha kifo cha msichana huyo na alikuwa hamfahamu kwani yeye
amekuwa akifika eneo lake la kazi majira ya jioni na kuondoka asubuhi.
Habari zaidi zinaeleza kuwa baada ya
kufichuka kwa tukio hilo ambalo lilifanywa siri na familia hiyo,mmoja wa
majirani alitoa taarifa kituo cha polisi na askari polisi waliokuwa doria walifika
nyumbani kwa mtuhumiwa.
Mmoja wa askari polisi aliyefika nyumbani
kwa mtuhumiwa kwa lengo la kufanya uchunguzi,ambaye hakutaka jina lake litajwe
gazetini,alisema baada ya kufika katika nyumba hiyo siku hiyo, majira ya usiku
walitumia zaidi ya saa moja kugonga lango la kuingilia bila kufunguliwa licha ya kujitambulisha wao ni
askari polisi.
Alidai kuwa baadae askari hao walitishia
kuvunja mlango ndipo mtoto mmoja alifika na kufungua lango hilo,huku akiwaeleza
askari hao kuwa mama yake hayupo,hata hivyo askari hao wakiwa na silaha
waliamua kuingia ndani ndipo walipowakuta watuhumiwa hao wakiangalia mpira.
Askari hao waliondoka na watuhumiwa hadi
kituo kidogo cha polisi Mbauda ambako walitoa maelezo na baadae kudhaminiwa
baada ya kuwepo taarifa kuwa msichana
huyo alifariki kwa kifafa.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano
maalumu,mume wa mwanamke huyo,ambaye ni mfanyabiashara wa nguo za mitumba,John
Mwacha,,alieleza masikitiko yake sambamba na kukanusha madai yanayoelekezwa kwa
mkewe kuwa alimuua kikatili msichana
wake wa kazi.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus
Sabas,alithibitisha tukio hilo na
kuelezaa kuwa mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea nyumbani kwao wilayani
Muleba,mkoani Kagera kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment