Habari za Punde

Siku ya Kichocho ilivyoadhimishwa

 Mkuu wa Divishen ya Elimu Zanzibar Maalim. Ahmed Abdul-majid ambae ni Mgeni rasmin siku ya Kichocho Zanzibar, akihutibia wananchi na wanafunzi waliofika katika hafla hiyo huko Skuli ya Mwera Wilaya ya Magharibu Unguja ambapo kunasadikiwa kuwa na wingi wa Koa wambukizao Kichocho.
Wanafunzi wakionyesha picha jinsi ya maambukizi ya Kichocho yanavyopatikana, wakati wa maadhimisho ya Siku yaKichocho
 Sehemu ya wanafunzi waliofika katika sherehe ya siku ya Kichocho inayoadhimishwa kila mwaka hapa Zanzibar
 Wanafunzi wakionyesha picha jinsi ya maambukizi ya Kichocho yanavyopatikana. 
Sehemu wanaopenda kukaa Konokono wanaoambukiza Kichocho. Mto wa Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja.

5 comments:

 1. Mwera ni Wilaya ya Kat au Maghrib Unguja?? Nafikiri Mwera imo katika Wilaya ya Maghrib Unguja. Please counter check kwa wenye data za uhakika.

  ReplyDelete
 2. kuna haja ya kuwaelimisha hao wanafunzi kwamba hao konokono ni chakula kizuri na chenye lishe ya kutosha, wawatafute mtoni na kwa ajili ya chakula. Kwa kufanya hivyo watapunguza kichocho na kupata lishe. China wameondosha kichocho kwa kuwaelimisha wananchi wao umuhimu wa kuwatumia konokono kama chakula.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Je wewe unatumia?? na tayari umeshawaelimisha watoto/vijana wako kuhusu hilo?? Wachina na wengineo kutumia vyakula hivyo hakuvifanyi vyakula hivyo kuwa halali, kwa waislam ni kuangalia muongozo wa dini yao kuhusu vyakula, muongozo wa kiislam unatosha kabisa kwa imani yetu ya kiislaam. Tukiambiwa ni halali katika dini maana yake kuna faida na manufaa katika matumizi yake, na tukiambiwa haram basi kuna hasara na matatizo ndani yake.
   Wachina na wengineo wanatumia kaatika vyakula vyao mbwa, nyoka.......... hivi katika uislam ni haramu kwetu kuvitumia, hivyo nahisi tukitumia vigezo vya wengine katika vyakula nafikiri tutakwenda mchomo.
   Tufuate muongozo sahihi wa dini yetu katika vyakula na mambo yote maisha, na tutafanikiwa inshaallah

   Delete
 3. kitabu gani kilichokwambia konokono haramu, kuna tofauti gani ya konokono wa maji baridi na kome wa baharini. Halafu usiwe na jazba katika kuchangia mada nani kataja watu kula mbwa, usilete frustration zako za kidini katika mambo ya msingi.

  ReplyDelete
  Replies
  1. @ Anonymous June 22, 2014 at 9:15
   Wacha kukurupuka, hebu nawe tutajie hicho kitabu chake kinachosema konokono ni halali?? halafu mdau hapo juu hakuna sehemu aliyosema konokono ni haramu au halali, alilosisitiza ni kufuata misingi ya dini yetu kwa wenye kuamini basi.
   Sasa ikiwa wewe kwako mambo ya si ya msingi shauri yako. Mimi sijaona kama kuna jazba popote pale, bali wewe ndie uliyeleta jazba na kejeli au "Usilete frustration zako za KIDINI katika mambo ya msingi". Hivi mabo ya kidini si mambo ya msingi. Inna lillaahi wainna ilayhi raajioun.
   Mola atuhifadhi.

   Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.