Habari za Punde

20/06/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA WATU WA CHINA MH. LI YUANCHAO ANATARAJIWA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI ZANZIBAR 
TAREHE 25-26/06/2014

MAKAMU HUYO WA RAIS ATAPOKELEWA NA MWENYEJI WAKE MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDD UWANJA WA NDEGE WA ABEID KARUME SAA 10:00 NA BAADAE ATAFANYA MKUTANO NA MADAKTARI WA KICHINA VUGA MJINI ZANZIBAR.

MH. LI YUANCHAO PIA ATAFANYA PIA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDD HOTEL YA LAGEMA NUNGWI.
SIKU YA TAREHE 26/06 Mh. MH. LI YUANCHAO ATAENDA KUTEMBELEA MASHAMBA YA VIUNGO KIZIMBANI NA BAADAE ATAFANYA ZIARA KATIKA MAENEO YA MJI MKONGWE kabla ya KURUDI ZAKE MAJIRA YA MCHANA.

ILI KURAHISISHA ZIARA HIYO WAANDISHI WA KILA CHOMBO WATAKAOSHIRIKI ZIARA HIYO MNAOMBWA KUTHIBITISHA KWA KUTAJA MAJINA YENU ILI KUPANGA USAFIRI NA MAMBO MENGINE.
MWISHO WA KUWASILISHA MAJINA NI JUMATATU YA TAREHE 23

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.