TAARIFA KWA AJILI YA VYOMBO
VYA HABARI
·
Yazindua
nembo mpya, kauli mbiu na tovuti mpya.
·
Yatumia
teknolojia mpya ya 4G Wimax.
·
Ya
panga kuongeza usambazaji wa mkonge wake katika maeneo zaidi ya Zanzibar .
Zanlink kampuni inayoongoza katika
utoaji wa huduma ya internet leo rasmi imezindua chapa yake mpya, ambayo
inaashiriwa na utambulisho wa nembo mpya, kauli mbiu pamoja na tovuti yake
mpya.Mabadiliko haya ni taswira ya maendeleo ambayo Zanlink imekuwa ikiyapata
tangu ilipoanzishwa kiasi cha miaka 14 iliyopita.
Uzinduzi huu mpya ni uwakilishi mzuri wa
biashara na mabadiliko ya Zanlink katika mtazamo wa malengo ya mbele, muonekano
wake na ujumbe wake. Utambulisho huu mpya ni hatua madhubuti ya kuwafikishia
taarifa wateja waliopo na wateja watakao kuja kuwa sisi tunaendelea kutoa
huduma ambayo inawazidi washindani wetu.
Utambulisho mpya wa Zanlink ni wa kisasa
na unao waunganisha wateja katika hali ya kirafiki huku nembo yake ikiwa na
herufi za “Z” na “L” ambazo kwa pamoja huweza kuifanya Zanlink itambulike kwa
urahisi.
Chini ya mwamvuli huu mpya wa
utambulisho, kampuni imeamua kuyatumia maneno “keeping you connected” kama kauli yake mbiu ambayo itatumika katika matangazo
yake pamoja na katika shughuli zote za kuitambulisha Zanlink.
Kauli mbiu hii ni fupi lakini ni yenye
kuelezea malengo na mtazamo wa Zanlink wakati huo huo unasisitiza jambo ambalo
Zanlink hujitahidi kutekeleza kila siku kwa wateja wake.
Zanlink imechukua uwelekeo huu mpya kwa
kuzindua upya tovuti yake iliyofanyiwa mabadiliko ya www.zanlink.com ambayo inaonesha taswira mpya
ya Zanlink pamoja na huduma inazozitoa.
Tovuti hiyo imehusisha kwa kujumuisha
vitu ambavyo vinataarifu sifa na huduma za Zanlink, pamoja na ufanisi wake,
mazingatio na uhakika wa huduma. Tovuti hii
pia hutaarifu kuhusu uwajibikaji wa kampuni katika utoaji wa huduma zake
na katika kuisaidia jamii kama ambavyo imekuwa
ikifanya katika kipindi cha hivi karibuni.
Uzinduzi wa leo hauhusishi tu
ubadilishwaji wa utambulisho wa muonekano wetu wa kama
vile nembo, lakini pia unahusisha mabadiliko katika namna tunavyotoa huduma kwa
wateja wetu.
Utambulisho mpya pekee hautoweza
kuthibitisha uaminifu wetu katika utoaji wa huduma lakini tunaamini kwa dhati
kuwa chapa yetu mpya itatuhamasisha katika mipango yetu endelevu katika kutoa
huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu
Kuambatana na uzinduzi huu, kampuni
imeanza kutoa huduma yake mpya ya teknolojia ya 4G WiMAX ambayo hutumika kwenye
masafa ya 3.5 GHz ambayo ni masafa ya leseni na hivyo huduma itaweza kutolewa yenye
uhakika zaidi na isiyoingiliana na masafa mengine.
Mipango ipo pia ambayo inafanyiwa kazi
ya kuongeza mtandao wa kutumia mkonge katika maeneo zaidi ya Zanzibar . Mwanzoni mwaka huu, Zanlink
ilikamilisha kuweka kituo Tanzania
bara cha kutoa na kuunganisha huduma mbalimbali za “VLAN” na “Layer2”.
Kufanya haya yameipatia Zanlink wigo zaidi
wa kujenga mashirikiano ya kimkakati pamoja na watoaji huduma wa kimataifa
katika Afrika Mashariki.
Uzinduzi
wa chapa yetu mpya ya utambulisho utaanzisha awamu mpya itakayozungumzia sisi
ni nani kama kampuni. Tunajivunia kuwa mbele
ya wenzetu katika sekta hii, na chapa yetu mpya ya utambulisho itaonesha umbali
ambao Zanlink imetokea katika kipindi cha miaka 14 ya historia yake.
Tulianza kwa kutoa huduma kwa njia ya mawasiliano
ya simu na tukakua na kuweza kuwafikia 65% ya wateja wote waliyomo katika soko
kwa kutoa huduma mbalimbali zenye kuhitajiwa na wateja wetu. Wakati huo huo
tukiendeleza utoaji huo wa huduma huku tukiwazingatia na kuwathamini wateja
wetu kwa kuwahudumia katika viwango vya juu.
Chapa hii mpya tayari imeshaanza
kutumika katika namna zote za electronik kama
vile katika tovuti yetu, na pia katika mitandao ya kijamii na katika namna
nyenginezo za mawasiliano ya electronik na katika chapa mbalimbali.
Kuhusu ZANLINK
Zanlink ilianzishwa mwaka 2000 na ni kampuni yenye kuongoza katika
utoaji wa huduma Zanzibar
kwa kutoa huduma ya “broadband” kwa kasi zaidi pamoja na huduma nyenginezo za
kimtandao.
Zanlink imeweka mtandao wenye ubora wa hali ya juu ambao unajumuisha
mtandao wa mkonge katika mji na pia mtandao wa kutumia mionzi ambao unasaidia
utoaji wa huduma mbalimbali. Mtandao huu umesambaa katika maeneo mbalimbali ya
Unguja na Pemba .
Zee Communications LTD (Zanlink)
S.L.P 4024, Zanzibar ,
Tanzania
Simu: + 255 24 2237480/1. Barua pepe: info@zanlink.com. URL: www.zanlink.com
No comments:
Post a Comment