Na Mwandishi wetu
SHIRIKA LA Umeme Zanzibar (ZECO) limesema
kukatika umeme katika maeneo yote ya Unguja na Pemba, kulitokana na kuzimika
ghafla mitambo ya kuzalisha umeme Tanzania Bara.
Taarifa ya ZECO kwa vyombo, ilisema
kuzimika kwa mitambo hiyo kulisababisha kuondoka kwa gridi ya taifa ambayo Zanzibar inapata umeme
kupitia gridi hiyo.
Kutokana na tatizo hilo
maeneo yote ya Unguja na Pemba na baadhi ya mikoa mingi ya Tanzania Bara
yalikosa umeme.
Wakati akizungumza na kituo kimoja cha
habari nchini ,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi
Felchesim Mramba, alisema chanzo hasa kilichopelekea kuzimika kwa mitambo hiyo
bado hakijajulikana na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
ZECO limeelezea kusikitishwa na kukatika
kwa umeme huko kwani shughuli nyingi za kimaendeleo zilisimama ikiwemo wananchi
kukosa kutazama na kusikiliza maelezo ya moja kwa moja kutoka Baraza la
Wawakilishi, kuangalia fainali za Kombe la Dunia na kusimama kwa shughuli
nyengine za kimaendeleo.
Taarifa hiyo imesema Shirika litaendelea
kutoa taarifa za kina kwa vyanzo vyovyote vile vya kukatika kwa umeme na
kuwaomba wananchi kuwa wastahamilivu wakati wa matukio kama
hayo yanapotokea.
Aidha taarifa hiyo imewataka wananchi
kuacha vitendo vya kuhujumu miundombinu kwa kuchimba mchanga chini ya njia za
umeme.
Mtegemea cha Ndugu mwisho atalala njaa... Hivo Umeme Huo haukatiki mpaka Ramadhani hata Ramadhani+
ReplyDelete