Na Rose Chapewa, Mbeya
MWANAMME aliyefahamika kwa jina la
Kiswigo Anganisye (33) mkazi wa kijiji cha Ibungila, anashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za kumpiga fimbo mama yake mzazi
sehemu ya kichwani na usoni na kisha kumnyonga shingo na kusababaisha
kifo chake,baada ya kumpikia magimbi badala ya ugali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed
Msangi, mwanamke aliyeuawa ni Martha
Kyando (73) mkazi wa kijiji cha Ibungila.
Alisema tukio hilo lilitokea Julai mosi
mwaka huu majira ya saa 6:30 usiku
katika kitongoji cha Mpunguti kijiji cha Ibungila kata ya Malindo, tarafa ya
Ukukwe wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni baada
ya mama huyo kumpikia mtuhumiwa magimbi badala ya ugali, ambapo alichukia na
kumpiga mama yake.
Alisema uchunguzi unaonesha mtuhumiwa huyo
anasumbuliwa na ugonjwa wa akili, na kwamba bado uchunguzi zaidi unaendeea, ili
hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Katika tukio jingine watu wawili wanaodaiwa kuwa raia waMalawi
wanashikiliwa kwa kosa la kuingia
nchini bila kibali.
Aliwataja watu hao kuwa ni Thomas Juma
(29) na Bonophace Chitete (29), na kwamba walikamatwa Julai 1 mwaka huu majira
ya saa 5:15 wilayani Kyela baada ya jeshi hilo
kufanya msako maalumu.
No comments:
Post a Comment