Habari za Punde

Balizi Seif afutari pamoja na wananchi wa Nungwi

 Baadhi ya waumini na Wananchi wa Kijiji cha Nungwi  pamoja na Wilaya ya Kaskazini “ A “ wakifutari pamoja futari iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Kituo cha Afya Nungwi.

  Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “ B “ Nd. Khamis Jabir Makame kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pembe Juma Khamis na Wananchi wa Mkoa huo akitoa shukrani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif baada ya kuwaandali Futari ya pamoja.

Kushoto ya Nd. Khamis Jabir ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Seif na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji.
Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na baadhi ya wazee wa Kijiji cha Nungwi mara baada ya kufutari nao pamoja mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wananchi hapa Nchini wako katika maandalizi ya mwisho ya  kusherehekea siku Kuu ya Iddi el Fitri baada ya kumalizika  kwa ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
 
Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni miongoni mwa nguzo tano za Kiislamu zinazomuwajibikia Muumini wa Dini hiyo kuzitekeleza ikitanguliwa na Kuamini uwepo wa Mungu Mmoja na Mtume Muhammad { SAW } ni Mjumbe wake, kusimamisha sala tano kwa siku, na zile mbili za mwisho za kutoa zaka pamoja na Kwenda kuhiji Maka kwa muumini mwenye uwezo.
 
Ibada ya funga inafikia ukingoni kwa waumini wa dini hiyo wakikamilisha kufutari pamoja katika maeneo na vitongoji tofauti kama ilivyotokea kwa Wananchi wa Kijiji cha Nungwi pamoja na wengine wa Wilaya ya Kaskazini “A”, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yeye binafsi na wakeze wote wawili walishiriki kikamilifu kwenye futari hiyo  ilifanyika katika eneo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Nungwi.
 
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na wananchi wa Mkoa huo Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “ B” Nd. Khamis Jabir Makame alisema futari ya pamoja kwa waumini wa dini ya Kiislamu ni kitendo kilichoamrishwa na Mwenyezi Mungu.
 
Nd. Jabir alisema mfumo huo unaowakutanisha watu wa rika na jinsia tofauti hutoa fursa kwa watu hao mkubadilishana mawazo, kupeana nasafa, ushauri na hata kuonyana kwa yale mambo yanayokatazwa ndani ya vitabu vya Dini na maamrisho ya Muumba.
 
Mkuu huyo wa Wilaya ya Kaskazini “ B” alifahamisha kwamba  maamrisho ya  Dini yamekuwa yakihimiza kwa  waumini wenye uwezo kuwajibika ipasavyo katika kuwafutarisha waumini wenzao waliowazunguuka

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.