Habari za Punde

Balozi Seif ampa pole Katibu wa CCM M/Magharibi kwa kufiwa na Baba yake mzazi

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji na kumpa pole Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Al Hajj Mwangi Rajab Kundya baada ya kufiwa na Baba yake Mzazi.

Mzee Rajab Kundya amefariki dunia jana nyumbani kwa mwanawe Katibu huyo wa CCM Mkoa Mjini hapo Kianga Wilaya ya Magharibi  na mwili wake kusafirishwa kwa Boti kupelekwa Dar es salaam kwa hatua ya mazishi.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.