Habari za Punde

Mkundemba bye byeMtunda ambao ulipandwa Kundemba mnamo mwaka 1982-1983 na kubatizwa jina la Mkundemba Leo hii umetuaga rasmi kwa kukatwa kutokana na chini kuwa umeshaoza sana na kuhatarisha  usalama na amani kwa wakaazi wa hapo.

Mtunda huu ndipo lilipokuwa duka maarufu la Alwatan wa Kundemba Ali Kibanda.

Kwa wakaazi wa Kundemba walio ughaibuni ambao wanaufahamu vizuri sana mtunda huu ambao ulipandwa na Marehemu Hassan Wigi wakija kutembea  kwa leo wataona tofauti imetokea mtaani kwao

2 comments:

  1. Kwa sisi tuliopo ughaibuni hatutashangaa sana maana ni mabadiliko ndicho tunachokililia. Lakini madam Mkundemba umetoweka na bado jina la asili la mtaa lipo yaani KUNDE na MBAAZI(KUNDEMBA) basi tunapata moyo kuwa majina ya asili ya mitaa yetu kuwa yanaenziwa..Jee ile barabara hoi ya mika nenda miaka rudi imesawazishwa katika kiwango cha lami au bado iko vile vile dimbwi mtu?

    ReplyDelete
  2. Mimi ningemshauuri ndugu Muandishi au Zanzinews wapeleke Salamu zetu kwamba tunawaomba Wananchi wapande Mti mwengine kama vile Mkungu . Kata Mti Panda Miti..

    Mji wa Unguja Unakubwa na Desertfication na kuna Tsunami Inatabiriwa kuikumba tena Zanzibar baada ya Miaka 125 iliopita .. Mji wa Unguja uko Below Sea Level na Miti mingi imekua ikikatwa katwa bila ya Sababu na Mazingira wamekaa kimya..

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.