Na Fatina
Mathias, Dodoma
KUMEIBUKA
kundi la watu wanaowapotosha Waislamu kwa kuwataka wasiwapeleke watoto wao
skuli na vyuo vikuu na badala yake
wasome Quran pekee, kwa madai kwamba elimu ya vyuo vikuu ni ukafiri.
Hayo
yalielezwa jana na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Dk. Seif Sulley, wakati
akizungumza na wakazi wa mjini Dodoma.
Aidha
alisema kundi hilo limekuwa likiwahamasisha wanafunzi wa kiislamu walio vyuo
vikuu kukatisha masomo yao.
"Kwa
gharama yoyote ile nitajitahidi kupambana na kundi hili ambalo linaharibu
maisha ya watu,” alisema.
Alisema watu
hao wamekuwa wakipita vyuoni na kutoa kauli kama hizo misikitini na kuwaachisha
masomo wanafunzi.
Aliwataka
Waislamu kuwapiga vita watu hao kwa sababu hawana nia njema na Waislamu na
wanapotosha Uislamu ambao umehimiza watu kusoma.
Hao wanaofanya hivo Watakua Sio Waislamu Halisi bali ni Fanatical au Foundamentalistic muslim kama wale WATALABANI.... Quiran imeweka wazi kwamba Muislamu anatakiwa apate Elimu ya Dini na Dunia hata kama Elimu hiyo itakua inatolewa mbali na kutaja mfano wa umbali huo kua ni Uchina.
ReplyDeleteSasa hao Wanaokuja nakuwatia maneno Wazee kwamba watoto wasisome Elimu ya Dunia kwani ni Ukafiri.. Hao watoto wanaweza kupata kazi kweli na kuongoza Nchi yao ikiwa hawana Elimu nyengine baada ya elimu ya dini tuu.....
Tunatakiwa Watanzania Waislamu tusiwe wajinga kiasi hicho, na tutizame mfano mmoja ambao unaendelea kutokea katika Nchi ya Tanganyika.. Ni kwamba Nafasi zote kubwa za Serikali na Nyeti zimekua zikihodhiwa na Wakristo watupu hali yakua Waislamu wenye Elimu wapo.. Lakini Huu umekua ni Ubaguzi wa Mfumo Kristo wa Serikali ya Tanzania/ Tanganyika...
Sasa Wanapokuja Muslim Fanatical wakasema tusiwapeleke watoto mashule na badala yake tuwasomeshe Quran tupu..Hivo si tutazidi Kukosa hizo nafasi za uongozi katika Nchi?....
Mimi nawaomba Waislamu Wasome hata kozio za Upailot na Nyengine ambazo zinakua ni Gender..Muislamu anatakiwa kupata Elimu ya Dini na Dunia Kurani katika Sura til "Ikra" imesema hivo...