Na Joseph ngilisho, Arusha
MUFTI Mkuu wa Tanzania , Shekh
Issa Bin Shaaban Simba, amewaonya Waislamu wanaosababisha migogoro
misikitini na wakati mwengine kuteka viongozi wa misikiti.
Alitoa onyo hilo baada ya kutatua mgogoro wa uongozi
katia mskiti mkuu uliopo Bondeni manispaa ya Arusha.
Alisema kuna baadhi ya Waislamu wamekuwa
wakiitumia misikiti sehemu za migogoro na kupindia uongozi uliowekwa kisheria
kwa sababu zao binafsi.
Alisema hali hiyo mbali ya kusababisha
migogoro pia imeifanya misikiti kuwa na makundi mawili ya uongozi, jambo ambalo
halikubaliki.
Alisema kutokana na hali hiyo amelazimika
kufanya
ziara Mkoani Arusha na kukutana na
viongozi wa serikali,viongozi wa Bakwata
wa makundi yote yanayokinzana, ili kujaribu kumaliza mvutano.
Mufti Simba, alisema viongozi waliokuwa
wakishikilia msikiti huo hawana haki, badala yake wanaotakiwa kuwa viongozi ni Sheikh wa mkoa, Shaban Juma Abdallah, Kaimu Katibu
wa mkoa, Ustadhi Abdallah Masoud na Mwenyekiti wa halmashauri, Ustadhi Mohamed
Juma Marawi.
Aidha alisema baraza la Masheikh mkoa litaongozwa na Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni,Sheikh Nassib Idd
Nassib, Sheikh Hussein Said Ijunje,Sheikh Abdallah Hanafi Simba na Sheikh
Abdulrahman Salum.
Aliwataja wajumbe wanostahili kuwepo
kwenye halmashauri ya mkoa ni Hassan
Waziri Salum, Said Rashid Golugwa,Athuman Amir Yunus,Seif Juma Banka,Athuman
Juma Luwuchu, Mohamed Kidange Laizer, Salim Rajab Majaaliwa na Rashid Kilavo
Msuya.
Aliwahimiza Waislamu kuimarisha umoja na
mshikamano kwa kuwa uislamu ni dini ya amani na sio ya mivutano.
No comments:
Post a Comment