Habari za Punde

Ufafanuzi kuhusu aina za ajira zilizositishwa Idara ya Uhamiaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA YA KUSITISHWA KWA AJIRA ZA KONSTEBO NA KOPLO WA UHAMIAJI ILIYOTOLEWA JANA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI HAIHUSIANI NA AJIRA 70 ZILIZOTOLEWA KWA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI


Baadhi ya Vyombo vya Habari leo tarehe 29 Julai, 2014 vimeandika kwa makosa kuwa ajira za Uhamiaji zilizositishwa jana zinahusiana na 70 zilizopatikana baada ya usaili uliofanyika katika Uwanja wa Taifa.

Ukweli ni kuwa usaili wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji ambao awali ulianzia Uwanja wa Taifa ulienda vizuri hadi wakapatikana wasailiwa wa kujaza nafasi 70 za Mkaguzi Msaidizi wa
Uhamiaji. Zoezi hilo halikuwa na matatizo yoyote, na waliochaguliwa walitakiwa kuripoti kazini tarehe 29 Julai lakini kwa sababu ya Sikukuu sasa wataripoti baada ya sikukuu.

Hivyo tunapenda kufafanua kuwa wasailiwa waliochaguliwa kujaza nafasi 70 za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji hawahusiki na usitishwaji uliotangazwa jana na wanatakiwa kuendelea na mipango ya kuripoti kazini kama ilivyotangazwa hapo awali.

Wasailiwa wanaohusika na kusitishwa kwa ajira zao ni wale waliokuwa wameshiriki katika zoezi la kuajiri Konstebo na Koplo wa Uhamiaji ambao idadi yao ni 200, ambao walitakiwa kuripoti tarehe 06 Agosti, 2014 lakini kwa sasa hawa ndio wanaelekezwa wasubiri hadi hapo watakapopewa maelekezo mengine.

Sgn
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
29 JULAI, 2014

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.