Habari za Punde

Balozi Seif atembelea maonyesho ya biashara ya Eidul Fitr Maisara

 Mwakalishi wa Kampuni ya Simu ya TTCL Kanda ya Zanzibar Mohd Yussuf Mohd akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mfumo mpya wa matumizi ya mawasiliano unaotumiwa na Kampuni hiyo kwa wateja wake.
 Afisa Uhusiano msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Ispector Sharif Bakar Sharif akimpatia ufafanuzi Balozi Seif juu ya mabadiliko ya pasi za kusafiria ambayo  yako katika kiwango cha teknolojia ya kisasa Kimataifa.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia bidhaa za chai ya Tanzania zilizofungwa kitaalamu kwa mauzo na Jumuiya  ya ZAPETA FOOD.
 Balozi Seif akifurahia bidhaa za mikono zilizotengenezwa na Jumuiya ya Princes Nadia huku Meneja mauzo wa Jumiya hiyo Saleh Shamte akipatia maelezo ya kina ya harakati zao za uzalishaji.

 Vijana Hidaya Hassan na Flora Mweipas wa Kikundi cha watu Vijana watano wanawake wasiosikia  kutoka Dar es salaam wakiwa na Mkalimali wao aliyepo kati kati yao Makame Ali wakimpatia maelezo ya miradi wanayoifanya  Balozi Seif aliyefika kungalia maonyesho ya Biashara ya Idd El Fitri hapo Maisara Suleiman Mjini Zanzibar.

 Balozi Seif akifurahia bidhaa za Pili pili, achari na tomato zinazotengenezwa na Kampuni ya Zanto Food Product iliyopo Viwanda vidogo vidogo hapa Zanzibar.

Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Thuwaiba Kisasi.
Bibi Salma Othman Mohd wa Jumuiya ya Dawa asili ya Meli Nne Herbal Product akimpatia Dozi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif juu ya huduma za dawa wanazotowa kwa jamii katika maeneo mbali mbali Nchini.


Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.