Habari za Punde

Makocha kutoka Barcelona wawasili kutoa mafunzo Dar

 
Balozi wa Hispania nchini Tanzania Mh.  Luis Manuel  Ceuesta Civis  (Kulia) akiongea na Makocha kutoka Timu ya Barcelona ya nchini Hispania katika mkutano wa Wanahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana (leo), makocha hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo ya siku mbili kwa makocha wazalendo, wa kwanza kushoto ni Kocha Daniel Bigas Alsina  na katikati ni Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes

 
: Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda (Katikati) akiongea na Wanahabari (Hawapo pichani) kuhusu  makocha wa Timu ya Barcelona  kutoka nchini Hispania  ambao wako nchini kwa ajili ya  mafunzo ya makocha yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili, wa kwanza kulia ni Balozi wa Spain nchini Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis, mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano na Kiwanda cha Bia cha Tanzania Breweries.

Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes (katikati)   kutoka timu ya Barcelona ya nchini Hispania (katikati) akitoa maelezo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya siku mbili watakayotoa kwa makocha 30 wakizalendo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bi. Juliana Yassoda na wa kwanza kushoto ni kocha Kocha Daniel Bigas Alsina 
Makocha wa Kizalendo 30 ambao wanatarajiwa kupewa mafunzo ya siku mbili kutoka kwa makocha wa Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja
Picha zote na Benjamin Sawe kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHVUM

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.