Mama
Shujaa wa Chakula 2014 Bi. Bahati Muriga akitoa neno la Shukurani Baada ya
Kukabidhiwa zawadi rasmi zawadi zake Wilayani kwake Ukerewe
Bi.Eluka Kibona kutoka Oxfam akimkabidhi ufunguo wa Pikipiki Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula
Mama
Shujaa wa Chakula 2014 Bi.Bahati Muriga akisaini kupokea zawadi zake
kutoka OXFAM kupitia Programu ya GROW, Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo
Inalipa.
Bwana
Hamis Kombo muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe akitoa salamu za
pongezi kwa Mama Shujaa wa Chakula 2014 pia kuwashukuru OXFAM kwa kutoa
zawadi hizo.
Bi.Bahati Muriga akijaribisha kuiwasha Pikipiki yake Mara baada ya Kukabidhiwa, baada ya kuibuka mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula Tanzania kwa mwaka 2014.
Kulwa Kizenga wa kwanza kushoto na Eluka Kibona kutoka OXFAM wakimkabidhi zawadi Bahati Muriga
Zawadi alizokabidhiwa mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka 2014.
Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2014 lilifikia tamati mnamo tar. 18 May, 2014 ambapo Bahati Jacob Muriga ndiye aliyeibuka kidedea wa shindano hilo. Mama shujaa huyu ni mkulima kutoka Nansio, Ukerewe mkoa wa Mwanza na pia ni mwalimu mkuu shule ya Msingi Mhozya. Ni mjane mwenye watoto watatu na hutumia kilimo kama nguzo ya kuhakikisha mahitaji ya kifamilia yanatimizwa.
Hafla
fupi ya kumkabidhi zawadi zake Bahati zilifanyika katika Ukumbi wa Afro Beach ambapo
watu na wawakilishi mbali mbali kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya
kiserikali kama vile Kivulini, EMEDO walihudhuria ili kushuhudia jinsi anavyokabidhiwa zawadi.
Bw.
Kombo, akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ukerewe alionesha furaha yake kwa mama
shujaa kutoka Ukerewe alisema” Ninayo
furaha kubwa na kama kiongozi kijana kuona wilaya yetu imetoa mshindi wa
shindano kubwa kama hili na kuiweka ukerewe katika historia na ramani ya nchi kuwa, kumbe nasi tunaweza,
najisikia furaha pia kwa ushindi huu kwani toka anaanza huu mchakato wa
kuchukua fomu na kuelekea kijiji cha maisha plus nilikua miongoni mwa niliotoa
ushirikiano mkubwa kwa kutoa ruhusa na araka
zangu za yeye kushiriki katika shindano hili kwani ni mwalimu huyu”
No comments:
Post a Comment