Wizara ya afya Zanzibar kwa kushirikian na Taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION wameendesha kambi ya matibabu ya midomo wazi katika hospitali ya mkoa Lumumba ikiwa ni muendelezo wa kambi zinazofanywa na taasisi hio ili kuhakikisha watoto wenye tatizo la midomo wazi wanapatiwa matibabu.
Akizungumza katika kambi hio Mkurugenzi na muazilishi wa Taasisi hio Dr Piter Mabula amesema takriban miaka kumi na moja taasisi hio imekua ikitoa huduma hio na imefanikiwa kufanya matibabu wa watu zaid ya 2500 kwa Tanzania bara na visiwani ambapo kwa zanzibbar zaid ya watu 200 wamepatiwa huduma hio
Dr.Piter Mabula Mkurugenzi wa
taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION
Kwa upande wake Dr Sumaiya Said Abud kutoka
katika hospitali ya mkoa Lumumba amesema kambi hio ya siku tano inatarajia
kufanya matibabu ya watoto 25 ambao tayar watoto hao wamefanyiwa uchunguzi wa
awali
Dr Sumaiya Said Abud hospitali ya
mkoa Lumumba
Sambamba na hayo sumaiya ametoa wito kwa wazazi
na walezi wenye watoto wenye tatizo la mdomo wazi kuwafiikisha katika hospitali
hio ili kupatiwa matibabu
CLIP… Dr Sumaiya Said Abud hospitali ya
mkoa Lumumba
Nao wazazi wa watoto waliopatiwa huduma hio
wameishukuru serikali ya mapinduzi ya Zanzibar pamoja na taasisi ya THE SAME
QUALITY FOUNDATION kwa kuwapatia huduma hio bure hali ambayo inawapa faraja ya
watoto wao,
No comments:
Post a Comment