Habari za Punde

Rais Dk.Shein awakaribisha Diaspora wa Zanzibar Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wazanzibari wanaoishi   nchi za nje (Diaspora)  wakati alipowaalika katika chakula maalum leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi mbali mbali (Diaspora)wakati alipowaalika katika chakula maalum leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika hafla ya chakula alichowaandalia  Wazanzibari wanaoishi Nchi za nje  (Diaspora)  katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo
Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) wakichukua chakula walichoaandaliwa na   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.[
Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) wakichukua chakula walichoaandaliwa na   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wazanzibari wanaoishi  Nchi za nje  (Diaspora) wakiwa katika chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Mshauri wa Rais  Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na  Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa alipokuwa akizungumza machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake kwa Wazanzibari wanaoishi  Nchi za nje  (Diaspora) aliowaalika chakula cha mchana leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,
Bi Hafsa Hassan Mbamba kwa niaba ya Wazanzibari wanaoishi  Nchi za nje  (Diaspora) akitoa neno la  shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   kwa mwaliko huo na kutoa pongezi kwa jitihada zinazo chukuliwa na Mheshimiwa Rais na Serikali yake kwa ujumla,baada ya hafla ya chakula katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wazanzibari wanaoishi  Nchi za nje  (Diaspora) wakiwa katika hafla ya chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Baadhi ya Wazanzibari wanaoishi  Nchi za nje  (Diaspora) wakiwa katika chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

27 comments:

  1. Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (Diaspora)?
    Heee? kwani kuna wazanzibar au watanzania wanaoishi nchi za nje? mara njingi tumekuwa tukiona viongozi wa Zanzibar au Tanzania kama akina wakifika nchini marekani au barani ulaya huwa wanapiga picha za pamoja na kuweka vikao na eti wanaoitwa waTanzania wanaoishi nje?
    je hawa Wazanzibar Diaspora au watanzania wanaoishi nje ni akina nani? uwe na sifa gani ili uwe ni mzanizibar au mtanzania unaeishi nje? uwe na vitambulisho vya aina gani ili ubakie kuwa mzanzibar au mtanzania unaeishi nje?
    mbona mara zote viongozi wanawakataa watanzania au wazanzibar wenye vitambulisho vya nje na kuwa wao sio wananchi halali wa nchi waliozaliwa,
    je hii si kinyume cha sheria ya Rais kuwaalika eti wazanzibar wanaoishi nje hali ya kuwa wananchi hao wanaishi nje na vitambulisho vya nchi za nje wanazoshi?
    mbona hizi siasa za kipumbavu zinatia kichefuchefu , ati unamkubali mtu na akiondoka tu unasema sio raia wa nchi, acheni upumbavu amkeni nyinyi mambumbumbu na siasa za kizamani,nchi zote duniani zinaendelea zikiwa na watu wenye uraia wa nje na wanchi yao,
    leo hii raisi anaawalika watu ambao sio raia wa zanzibar kisheria yaani anavunja sheria ya kuwaita raia hali sheria ya nchi ya Tanzania hao sio raia na hawaruhusiwi kupiga kura,
    acheni hizo nyinyi roho mbaya za kijinga eti mtu anaishi nje wewe inakuuma na kuona eti sio raia tena wa nchi yako lakini mtoto wako akiwa anaishi nje hali ya kuwa wewe ni kigogo wa nchi unamuita kuwa ni raia, na akirejea nchini anaweka uraia wake wa nje pembeni na wewe unampa buku la uzanzibar au utanzania na kuanza kugombea ubunge au uwakilishi hali ya kuwa yeye alikuwa anaishi nje na uraia wa nje vilevile akirejea nje anatumia uraia wake wa nje,
    mbona huyu raisi anaipinda sheria na kuwaalika watu ikulu wasiokuwa raia wa nje kwa mujibu wa sheria zenu za kiajabu ajubu za kipumbavu,
    acheni ujinga nyinyi, je sasa hawa sisi tuwatambue ni raia wa Zanzibar au ni raia wa nje wakio alikwa ikulu?

    ReplyDelete
  2. Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (Diaspora)?

    Heee? kwani kuna wazanzibari au watanzania wanaoishi nchi za nje? Mara nyingi tumekuwa tukiona viongozi wa Zanzibar au Tanzania wakifika nchini Marekani au barani ulaya huwa wanapiga picha za pamoja na kuweka vikao na eti wanaoitwa waTanzania wanaoishi nje.

    Je hawa Wazanzibari Diaspora au watanzania wanaoishi nje ni akina nani? Uwe na sifa gani ili uwe ni mzanzibari au mtanzania unaeishi nje?

    Uwe na vitambulisho vya aina gani ili ubakie kuwa mzanzibar au mtanzania unaeishi nje?

    Mbona mara zote viongozi wanawakataa watanzania au wazanzibari wenye vitambulisho vya nje na kuwa wao sio wananchi halali wa nchi waliozaliwa?

    Je hii si kinyume cha sheria ya Rais kuwaalika wazanzibar wanaoishi nje hali ya kuwa washaukana uraia wao kwa kuwa na Paspoti za nchi nyengine?

    Mbona mtu akiondoka tu unasema sio raia wa nchi, lakini hapohapo unamualika IKULU.

    Leo hii Mheshimiwa Rais anaawalika watu ambao sio raia wa Zanzibar kisheria Je Mheshimiwa Rais havunji sheria kwa kuwaita raia hali sheria ya nchi ya Tanzania hao sio raia na wala hawaruhusiwi kupiga kura?

    ReplyDelete
  3. Diaspora Department Mpo? Masuala hayo yanataka majibu

    ReplyDelete
  4. Nje ya Zazibar hakuna kitu kinachoitwa ''RAIA WA ZANZIBAR'' ila hutambulika kuwa wao ni RAIA WA-TANZANIA. Ifahamike kijiografia wazanzibari hutambulika uraia wao ndani ya mipaka ya United Republic of Tanzania. Nje ya hapo unatambulika kama Mtanzania,. It's just my interpretation comrade!

    ReplyDelete
  5. Napenda kujibu ipasavyo. Ingawa Katiba ya Zanzibar imetoa maelezo ya nani ni mzanzibari. Lakini hakuna utambulisho sahihi wa mzanzibari. Wazanzibari waliku wale ambao walizaliwa na kuwepo kabla ya mungano.

    Watu wote wanaoishi Zanzibar kwa sasa ni wakaazi wa Zanzibar wenye uraia wa Tanzania. Kuanzia Raisi hadi wanaozaliwa Leo ni wakazi tu wazanzibar. Huu ndio uhalisi yakinifu.

    Ni busara kwa raisi wetu kuweza kuwalika na kujumuika na kundi la watanzania wenye asili ya Zanzibar ambao wanaishi nchi za nje. Ghafla hii inathibitisha mapenzi ya dhati waliyonayo wakaazi wa Zanzibar waliopo Zanzibar na wazanzibari wasaka tonge waliosambaa kila kona ya dunia.

    ReplyDelete
  6. mdao hapo juu umeuliza masuali mazuri sana, sasa hawo wanaojiita diaspora tunaomba majibu, si mmeshaukana uzanzibari au utanzania nyinyi sasa mnajiita diaspora kwanza hiyo diaspora kirefu chake ni nini? ni jumuiya au? na mtu ili ajiunge anahitajika afanye nini? mbona kuna watu wengine wapo nje na hawaijuwi hii diaspora? inaonesha ni kiini macho cha wale walifukuzwa wakati wa mapinduzi kutaka kurejee tena, napata mashaka mbona hawa wengi ni wamanga? kama nitapatiwa majibu ya kuridhisha na mimi huenda nikawa mwanachama!

    ReplyDelete
    Replies
    1. wacha ujinga huo wengi wamanga unamjua mmanga wewe, wingi wamanga umepiga hesabu vipi?

      Delete
    2. nawajuwa wamanga ndio maana nikasema na huo sio ujinga kama mjinga ni wewe, nadhani unamacho angalia inaonesha wewe ndio hujuwi wamanga ni akinanani! usikuripuke fanya utafiti kwanza.. au kamuulize babu yako.

      Delete
    3. Nawajuwa wamanga ndio maana nikasema, kama mjinga ni wewe labda uelimishwe kidogo, neno wamanga sio matusi ni sawa nakusema wapemba ingawa baadhi ya watu wanakataa kuitwa hivyo ingawa wanaasili..

      Delete
    4. Muarabu hakai Zanzibar wewe ni Wamanga tu musione wanajiita waarabu hali ya kuwa ni Wamanga tu,takribani hakuna Mmanga yoyote hapo anaejua kiarabu kwa ufasaha labda baadhi wanaojifanya kusafiri na kuishi nje kidogo katika nch za Waarabu wenyewe wao ndio huwa wanajaribu cha kuombea maji huku ukiwaona hasa kikiwagonga ugokoni,
      nitajia mmoja kati hao wanaojiita waarabu anaejua kiarabu kuanzia watoto wao na wao wenyewe? ni Wamanga tu sio waarabu.

      Delete
  7. SMZ yaandaa sera ya diaspora kuvutia walio nje

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema tayari imeweka mazingira mazuri ambayo yatasaidia Wazanzibari waliopo nje ya nchi kuwekeza Zanzibar na kusaidia katika miradi mbalimbali. Hayo yalisemwa na Mshauri wa Rais anayeshughulikia vitega uchumi na uwekezaji Balozi Mohamed Ramia wakati akifungua mkutano uliowashirikisha Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi.

    Alisema tayari Serikali ipo katika mchakato wa kutayarisha Sera ya Diaspora ambayo itakuwa muongozo katika utekelezaji wa majukumu yao.

    Alisema tangu kuanzishwa kwa Idara ya Diaspora mara baada ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein alipoingia madarakani mwaka 2010, Idara hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuwashawishi wananchi wengi wenye asili ya Zanzibar kusaidia maendeleo ya nchi.

    Mkurugenzi wa diaspora Khamis Mohamed alisema matayarisho ya Sera ya Diaspora ipo katika hatua za mwisho kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi mjini hapa.

    Alisema sera hiyo itasaidia kuweka mazingira mazuri ambayo Wazanzibari waliopo nje watakuwa na fursa na nafasi nzuri ya kutoa mchango wake kwa taifa.

    Mzanzibari anayeishi nchini Sweden, Mohamed Saleh alisema kuwepo kwa sera kutakuwa chachu ya kuleta maendeleo na wananchi kuchangia maendeleo ya taifa.

    Kwa mfano alisema Wazanzibari waliopo nje wanahitaji kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari ambavyo vitatoa nafasi kama utambulisho wa kushiriki maendeleo ya Zanzibar.

    “Sisi Wazanzibari tuliopo nje ya nchi tunahitaji kutambuliwa rasmi ikiwemo kupata kitambulisho cha Mzanzibari mkazi ambacho kitatupa nafasi ya kushiriki maendeleo ya taifa,” alisema.
    Idara ya Diaspora tayari imefanya ziara zaidi ya nchi tano kwa ajili ya kuwasiliana na Wazanzibari waliopo nje ya nchi kusaidia maendeleo ya taifa.

    ReplyDelete
  8. Waloko nje ni watoto wetu wa kizanzibar na hata hao viongozi wote wa Zanzibar watoto wao wako nje hususani Uengereza na Marekani na wana raia za nje , sasa vipi unaweza kuwatenga watoto wetu na wazazi wao tuloko Zanzibar?

    Baado Zanzibar na viongozi wake hawajafikia kutumia Sheria za Israil kua Wapalestina waloko nje ya Palestina hawana haki yakurudi Palestina na kujumuika na Familia zao na asili zao.

    ReplyDelete
  9. Mawazo ya Mhe. Ramia juu ya DIASPORAS ni mazuri lakini sidhani kama yanaweza kuzaa matunda tunayoyatarajiwa kwa mazingira yetu ya siasa za Z'bar.

    Muwekezaji siku zote hutarajia kupata faida kutokana na biashara yake na hii hutegemeana na uhuru alionao ktk kuendesha biashara yenyewe.

    Niliwahi kusikia kwamba hospitali ya AL-RAHMA ni miongoni mwa uwekezaji wa W'bari waishio nje na walikua na mkakati wa kuanzisha baadhi ya vitengo vya magonjwa sugu ili kuwapunguzia ndugu zao gharama za kwenda Bara.

    Lakini sakia, wakati wa machafuko ya mwaka 2000 walipewa ILANI juu ya kuwapokea majeruhi au kuruhusu kuongea na waandishi wa khabari.

    Sasa sijui kama tutakua tumebadilika au laa!

    ReplyDelete
  10. Diaspora ni kitendo cha mwananchi au wananchi wa nchi fulani kukimbia kwao na kwenda kuishi nje ya nchi hiyo,kwa sababu mbali mbali zikiwemo za kisiasa,kiuchumi,za kijamii na mengineo.Tukirudi kuangalia kwa upande wa Zanzibar,wengi walio nje wameamua hivyo kutokana na mambo mawili muhimu.Mojawapo ni Usalama wa roho zao kama tulivoshudia January 2001 huko Pemba.La pili ni chuki za kisiasa na la muhimu pia ni sababu za kiuchumi kama ilivyotokea katika kipindi cha udhibiti wa biashara serikalini.Hawa walio vuuka bahari katika hali ngumu walifanya hivo ili kjinusurisha nafsi zao na pia kupata mwanya wa kuweza kuwasaidia wazee,ndugu na hata jirani waliowaacha nyuma.Tunashukuru saana kwa michango ya wenzetu waliowahi kwenda nje la si hivo basi shida tuliokuanazo nyuma ingekua hazisemeki.Hawa wenzetu wanafungu lao katika nchi yao walikozaliwa wao na wazee wao.

    ReplyDelete
  11. @ Anonymous 1, .. Masuali yako uliouliza unaweza kupata majibu kama utajuwa masuali haya na kujipa jibu mwenyewe:

    a. Nini maana ya NENO TANZANIA?... Limetoka Wapi na ni kwanini?.....

    b. Kwanini Watu wanaotoka Bara wanangangania neno Tanzania ?......Jeee hawana asili nyengine zinazojenga historia ya utamaduni wao?????..

    c. Kwanini Watu wanaotoka Zanzibar hata wakiwa Nje ya Nchi wanajulikana kwa jina la Zanzibar na kujitambulisha Wenyewe kama Wazanzibari????

    d. TANZANIA imertoka Wapi? ...Na Kwanini Ikawa Kuna Watu wanajiita Watanzania na Wengine Wanaukana Utanzania huo?...

    Jibu langu moja ambalo litakusaidia kukupatia clue ya masuali mengine ni:

    Zanzibar ni Nchi Iliokuwepo kabla ya hiyo Tanzania unayojivunia wewe... Angalia Historia ya Wazanzibari na Identity yao... Laa Tanzania ni Neno la Kisiasa lilojengeka baada ya MUUNGANO Wa Serikali Tukufu ya Watu wa Zanzibar na Serikali tukufu ya Watanganyika.... Na kama kweli wewe ni mtu uliekwenda shule , hebu Soma Viini Macho vya Muungano huo.. Mfano mdogo ni ule ulioko Dodoma sasa hivi na masuali ya Jaji Joseph Sinde warioba ambayo aliwauliza wenzake wa CCM ...

    Hivo ndio maana Wazanzibari wanaitwa Wazanzibari na hata Wakiwa Nje wazanzibari wana Organisation zao za Kizanzibari hata kama kuna organisation za Kitanzania lakini Wazanzibari hawariziki mpaka wawe na zao... Kwani wanajua kwamba Tanzania ni neno la Kisiasa tuu ambalo kwa luha ya rahisi ni TANGANYIKA KUJIVISHA KOTI LA TANZANIA...

    .Hee mimi nakushangaa wewe ni Kijana au ni Mzee ambae nafikiri hata shule hujawahi kufika.... Nikisema hivo namaanisha kwamba Tanzania ni Neno la Kisiasa ndio munalojivunia Nyinyi Watu wenye asili Ya BARA ( Tanganyika).......

    Kwa Mzanzibari yoyote alieko Nje na Ndani ya Zanzibar anajuwa nini maana ya Kuwa Mzanzibari na Ndio maana hata Raisi amethamini hayo...... Zanzibar sio Neno la Kisiasa kama hiyo TANZANIA unayojivunia...

    @ Anonymous3 : Unasema Wazanzibari hawatambuliki Nje ya United Republic of Tanzania.. Huo ni Uongo Mzanzibari anatambulika kila corne ambazo ziko Western. Labda Nchi za Eastern Europe hawajui Zanzibar kwasababu Serikali ya Tanganyika kwakuvaa Koti la Muungano imeifuta Zanzibar katika International code... Lakini sasa hivi Nchi nyingi Wanaijua Zanzibar baada yakusoma historia yake...

    @ Anonymous 4 na 5.. Nyinyi kweli ni Vingunge wa Steven Wasira na Peter Pinda whom they think that Zanzibar will one Day be swollow by Mighty Tanganyika for so call One State of Tanzania.... Masuali na majibu yenu yanaonyesha kama kwamba Hamukupata kuenda shule au kusoma magazeti, kusikiliza redio, TV au intarnet media. If so will you offcourse Excused me by said so........Kama mumesoma habari kupitia kitengo japo kimoja cha hivo nilivovitaja musingeandika maneno ya kijinga kama hayo.. Lakini Tunawajua nyinyi ni nani hata mukasema hayo.. nini maana ya DIASPORA. munaweza kupata maana hiyo ikiwa muta google na mfano mzuri wa Diaspora ni huyo Msichana anaeitwa Hafsa.. Amezaliwa Denmark akiwa ni Mzanzibari baba na mama. Amesoma UK na amerudi Nyumbani sasa anasomesha..

    hata kama Wazee wake waliondoka au kukimbia 1964 kama mmoja wa nyinyi anavosema, lakini bado ni Wazanzibari na Zanzibar ni Nchi Iliokuwepo hapo mwanzo kabla ya Tanzania yenu ya Bandia... Na Zanzibar na Wazanzibari wataendelea kuwepo Dumu Daima mpaka Dunia Ifike mwisho..

    Kuhusu kuwa na Pasport nyengine ambazo sio za Tanzania.. What is Tanzania by the way?.... Tanzania Munaijuwa nyinyi tu sio wazanzibari.. Siasa hizo zenu ndizo zilizoifanya Ethiopia kufa Njaa miaka ya 70s-80s kwakuwanyima haki za kiraia Raia wao wa ethiopia waliokimbia mika ya Nyuma.. leo ethiopia na India ni Mfano wa nchi wanaothamini raia zao.... By the Way kutokana na Sheria za Kimataifa Uraia wa Kuzaliwa hauwezi kuepukika.. Na wenzetu Wa nchi tunazoziita (zimeendelea) Wanathamini hilo.. Wanaweza kukunyima kitu wewe muhamiaji na wakampa yule Mzaliwa..

    ReplyDelete
  12. @ Anonymous 1, .. Masuali yako uliouliza unaweza kupata majibu kama utajuwa masuali haya na kujipa jibu mwenyewe:

    a. Nini maana ya NENO TANZANIA?... Limetoka Wapi na ni kwanini?.....

    b. Kwanini Watu wanaotoka Bara wanangangania neno Tanzania ?......Jeee hawana asili nyengine zinazojenga historia ya utamaduni wao?????..

    c. Kwanini Watu wanaotoka Zanzibar hata wakiwa Nje ya Nchi wanajulikana kwa jina la Zanzibar na kujitambulisha Wenyewe kama Wazanzibari????

    d. TANZANIA imetoka Wapi? ...Na Kwanini Ikawa Kuna Watu wanajiita Watanzania na Wengine Wanaukana Utanzania huo?...

    Jibu langu moja ambalo litakusaidia kukupatia clue ya masuali mengine ni:

    Zanzibar ni Nchi Iliokuwepo kabla ya hiyo Tanzania. Angalia Historia ya Wazanzibari na Identity yao... Tanzania ni Neno la Kisiasa lilojengeka baada ya MUUNGANO Wa Serikali Tukufu ya Watu wa Zanzibar na Serikali tukufu ya Watanganyika.... Na kama kweli wewe ni mtu uliekwenda shule , hebu Soma Viini Macho vya Muungano huo.. Mfano mdogo ni ule ulioko Dodoma sasa hivi na masuali ya Jaji Joseph Sinde warioba ambayo aliwauliza wenzake wa CCM ...

    Ndio maana Wazanzibari wanaitwa Wazanzibari na hata Wakiwa Nje wazanzibari wana Organisation zao za Kizanzibari hata kama kuna organisation za Kitanzania lakini Wazanzibari hawaridhiki mpaka wawe na zao... Kwani wanajua kwamba Tanzania ni neno la Kisiasa tuu


    Kwa Mzanzibari yoyote alieko Nje na Ndani ya Zanzibar anajuwa nini maana ya Kuwa Mzanzibari na Ndio maana hata Raisi amethamini hayo...... Zanzibar sio Neno la Kisiasa kama hiyo TANZANIA

    @ Anonymous3 : Unasema Wazanzibari hawatambuliki Nje ya United Republic of Tanzania.. Huo ni Uongo Mzanzibari anatambulika kila corner. Labda Nchi za Eastern Europe hawajui Zanzibar kwasababu Serikali ya Tanganyika kwakuvaa Koti la Muungano imeifuta Zanzibar katika International code... Lakini sasa hivi Nchi nyingi Wanaijua Zanzibar baada yakusoma historia yake...

    Maana ya DIASPORA. munaweza kupata maana hiyo ikiwa muta google na mfano mzuri wa Diaspora ni huyo Msichana anaeitwa Hafsa.. Amezaliwa Denmark akiwa ni Mzanzibari baba na mama. Amesoma UK na amerudi Nyumbani sasa anatumikia nchi yake walipozaliwa wazazi wake.

    Hata kama Wazee wake waliondoka au kukimbia 1964 kama mmoja wa nyinyi anavyosema, lakini bado ni Wazanzibari na Zanzibar ni Nchi Iliyokuwepo hapo mwanzo kabla ya Tanzania ... Na Zanzibar na Wazanzibari wataendelea kuwepo Dumu Daima mpaka Dunia Ifike mwisho..

    Kuhusu kuwa na Pasport nyengine ambazo sio za Tanzania. Siasa hizo ndizo zilizoifanya Ethiopia kufa Njaa miaka ya 70s-80s kwa kuwanyima haki za kiraia Raia wao wa Ethiopia waliokimbia miaka ya Nyuma.. leo Ethiopia na India ni Mfano wa nchi wanaothamini raia zao....

    By the Way kutokana na Sheria za Kimataifa Uraia wa Kuzaliwa hauwezi kuepukika.. Na wenzetu Wa nchi tunazoziita (zimeendelea) Wanathamini hilo.. Wanaweza kukunyima kitu wewe mhamiaji na wakampa yule Mzawa.

    ReplyDelete
  13. Mtatuwia radhi huu ni mjadala muhimu na mzuri kwa hivyo baadhi ya comment tumezichuja ili ziende sambamba na maudhui halisi ya mjadala wenyewe na pia kuepusha mivutano na malumbano yatakayotutoa katika hoja. Tuendelee

    ReplyDelete
  14. Naona kama nduguyangu anonymous hujaelewa maana ya Diaspora wa Zanzibar!! Labda tukusaidie! Diaspora maana yake ni watu wenye asili ya pahali Fulani lakini wanaishi nchi nyengine. Hivyo, Diaspora wa Zanzibar haina maana ya raia wa Zanzibar!! Hawa ni watu wenye asili ya ZANZIBAR lakini wanaishi nchi za nje, wanaweza kua bado no raia wa nchi hii au wameshachukua uraia wa nchi wanazoishi!!! Na Rais hana kosa kumualika chakula mtu yeyote Ikulu awe raia au asiwe raia, huu ni uungwana tu, sio suala la kisheria nduguyangu. Usichanganye choko na mbaazi!!!!��

    ReplyDelete
  15. Naona kama nduguyangu anonymous hujaelewa maana ya Diaspora wa Zanzibar!! Labda tukusaidie! Diaspora maana yake ni watu wenye asili ya pahali Fulani lakini wanaishi nchi nyengine. Hivyo, Diaspora wa Zanzibar haina maana ya raia wa Zanzibar!! Hawa ni watu wenye asili ya ZANZIBAR lakini wanaishi nchi za nje, wanaweza kua bado no raia wa nchi hii au wameshachukua uraia wa nchi wanazoishi!!! Na Rais hana kosa kumualika chakula mtu yeyote Ikulu awe raia au asiwe raia, huu ni uungwana tu, sio suala la kisheria nduguyangu. Usichanganye choko na mbaazi!!!!��

    ReplyDelete
  16. Naona kama nduguyangu anonymous hujaelewa maana ya Diaspora wa Zanzibar!! Labda tukusaidie! Diaspora maana yake ni watu wenye asili ya pahali Fulani lakini wanaishi nchi nyengine. Hivyo, Diaspora wa Zanzibar haina maana ya raia wa Zanzibar!! Hawa ni watu wenye asili ya ZANZIBAR lakini wanaishi nchi za nje, wanaweza kua bado no raia wa nchi hii au wameshachukua uraia wa nchi wanazoishi!!! Na Rais hana kosa kumualika chakula mtu yeyote Ikulu awe raia au asiwe raia, huu ni uungwana tu, sio suala la kisheria nduguyangu. Usichanganye choko na mbaazi!!!!��

    ReplyDelete
  17. Oya, Oya, nyinyi nyote hamujui nini maana ya Diaspora, maana yake bwana ni changa la macho,
    ni baadhi ya watu waliokuwa karibu sana na watu wenye mtumbo manene hapo serikalini,bungeni au baraza la uwakilishi,ambao kwa makusudi tu wanawatumilia hao jamaa ambao walipanga hilo jina ili wazidi kuzimaliza hizo pesa zilizobakia hapo zanzibar,hao jamaa wanakuwa wakitiliwa fungu lao kila kukicha n mwisho wakajifanya eti wanatoa msaada kidogo kumbe wanakupigeni changa la macho kuwa zimetoka kwao, hebu niambie kuna mbeba boksi gani atafanya hivyo?hio hela inatoka hukohuko na kujaa katika acount zao na mukitaka kunichafua nitataja jina la mtu ambae alikuwa anabeba boksi U.K ambaye mwisho amekuwa ni jamaa wa karibu wa damu na kiongozi mmoja mkubwa sana hapo zanzibar ambae mwanzo wake alianzia huo mchezo wa diaspora na kuramba DUME .

    ReplyDelete
  18. Kule U.K wapo wale wanaojiita Tawi la CCM,ambao kila mara wanafanya mikutano na kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania pamoja na balozi wa Tanzania pale U.K na jamaa karibu wote wale hawabebi tena boksi wala nini,wanaingiziwa tu kutopa nhini kwao,huku jamaa wale wakiwa wanaishi U.K kama raia wa pale lakini wanavuta kutoka katika serikali kama wafanyakazi vile,na wanapeana kadi za uraia wa CCM pale na huku tukiambiwa kuwa raia wa nchi mbili hawatakiwi,na tusishangae kama wale wana CCM wanaopeana kadi za uraia kule Uk kama hawaji kupiga kura hapo nchini bila tatizo lolote yaani.

    ReplyDelete
  19. Uwekezaji ni pamoja na ujenzi wa nyumba bora na za kiasasa, ningependa kujua ni kwa kiasi gani SMZ imetenga maeneo maalum kwa ajili ya DIASPORAS?

    Kama SMZ imefanya hivyo, itasaidia sana kuboresha mandhari ya mji wa Z'bar na kupafanya mahala bora zaidi kwa wawekezaji wengine.

    Leo hii vijana wengi wanaotuma fedha nyumbani ili watafutuwe viwanja na wajengewe nyumba huishia maeneo yasiyo rasmi na wanaporudi hupigwa na mshangao!

    ReplyDelete
  20. Oya, Oya, nyinyi nyote hamujui nini maana ya Diaspora. Maana yake bwana ni changa la macho,
    ni baadhi ya watu waliokuwa karibu sana na watu wenye matumbo manene hapo serikalini,bungeni au baraza la uwakilishi,ambao kwa makusudi tu wanawatumilia hao jamaa ambao walipanga hilo jina ili wazidi kuzimaliza hizo pesa zilizobakia hapo zanzibar.

    Hao jamaa wanakuwa wakitiliwa fungu lao kila kukicha na mwisho wakajifanya eti wanatoa msaada kidogo kumbe wanakupigeni changa la macho kuwa zimetoka kwao.

    Hebu niambie kuna mbeba boksi gani atafanya hivyo?hio hela inatoka hukohuko na kujaa katika account zao

    ReplyDelete
  21. Sasa huyo Rais alipowaalika hao madiaspora walipita hapo na vitambilisho gani?

    Kama vya nje basi hao ni raia wa nje, na kama ikitokezea suala lolote la kiajabu ajabu ubali wa huyu unaemuita Diaspora wako utamchukua nchini kwake kwani ni raia wake na tutaachwa mimi na wewe tuendelee kutiliana unafiki.

    Tunaona baadhi ya haohao wanapofika uwanja wa ndege na kubainika kama ni mzanzibari lakini ana pasport ya nje,hao wahusika wa hapo ndio wanapozidi choyo chao cha roho mbaya na kuruhusu bwana mzungu apite na huku unaomtolea meno machafu kama " MAHINDI YALIYOPEA"

    Na ukimuona mwenzako ati yeye sio katika hao wanaojiita diaspora wanaotumia mgongo wa wakuu fulani ndani ya serikali "SIRIKALI" wao ndio wananyanyaswa na wala hawatakiwi kujulikana kama nao ni wazanzibar wanaotafuta Tonge yao pamoja na jamaa zao huko nje kama akina Hafsa na wengine uliowataja.sasa akina mwajuma wanaoishi nje na hawako katika hio diaspora wao hawana haki?

    ReplyDelete
    Replies
    1. @ Anonymous 17
      Hayo unayosema ya Uwanja Wa Ndege kunyanyaswa wazanzibari imeshatokea mara nyingi tu, lakini wanyanyasaji mara nyingi huwa wale watu wanaofanya kazi ktk Idara ya Uhamiaji ( mambo ya Ndani)... Mimi nimeshawahi kumkuta mmoja wao anawanyanyasa wasichana wa kizanzibari ambo walikua wanatoka Uk na wamekuja kutembea...

      alikua anawauliza kwanini wana passport za UK? ...maofisa wa Uhamiaji wanaofanya Roho mbaya ni wale kutoka Vyama vya CCM na wanawafanyia wananchi wadogo wadogo, watoto wa wakubwa hawawachezei.... Au wafanyakazi wenye asili ya Tanganyika na wao wanapenda kusumbua watu wenye asili ya Zanzibar. Ndio maana watu wengi wanagoma kupitia DSM.

      .Ilipofika zamu yangu licha ya kwamba ndani ya Passport yangu imeandikwa nimezaliwa Zanzibar alianza kuniuliza nina passport ngapi... Nikamwambia kazi yako sikuniuliza mimi niko na passporti ngapi bali nikunigongea muhuri wakutoka..

      akaanza kuniletea Ubabe nikampasha na nikamwambia nikikosa ndege yangu basi utanilipia ndege nyengine ili niondoke kwani hata Visa ilikua inamaliza siku 3 Mbele...

      Kuhusu diaspora Raisi Alituma Ujumbe wake Kule Copenhagen ili kufanya tathmini yakutaka kuweka Sheria mpya inayoweza kuwasaidia Wazanzibari (Diaspora) wanapoingia Nyumbani wasi-sumbuliwe na Immigration control.

      Katika Policy itakayoundwa kuhusu diaspora ni yakupatiwa Vitambulisho vya Mzanzibari ambavyo vitakua na rangi tofauti na Vitambulisho vya ZID.... Ambavyo ndani vitakua vimeandika Diaspora.. nk.... Hivi vitakua na Visa ambayo haina limitation ikiwa kama mtu anakusudia kuja kuwekeza Nyumbani....

      Mpango huu ni mzuri ambao hata Wa Ethiopia wanautumia, hivi sasa Ethiopians Diaspora wameshafanya hata Mobile Library ambazo zinakwenda mpaka Vijijini ( Milimani9 ambako watoto walikua hawana hata vitabu vyakusomea...

      Scandanevian Diaspora kutoka kwa www.zandias.org tayari wameshasaidia Sana Library ya Zanzibar.. Kila Mwaka huleta Vitabu na walimu ambao wametiliana saini na Baadhi ya Organisation kule Scandanevia..

      Ddiaspora ya Canada na wao wameshafanya hata michango yakujenga Hospitali au ku-repear hospitali ambayo inajiita www.zacadia.org... Wacanada kuna mmoja wa diaspora amefanya Project yakujenga upya ule msikiti wa Kizimkazi ambao ulijengwa na Wa Iran... Na hivi sasa Msikiti wa Kizimkazi au Unguja Ukuu unate,belewa na watalii wengi.. nimeona hata doccumentary kwenye CNN kuhusu Historia ya Tumbatu na Unguja Ukuu na Kizimkazi... Na Diaspora Wa UU na wao wanafanya mengi hata huko UK Wazanzibari wanamiliki jengo lao ambalo nusu ni Msikiti na nusu ni Madrassa ya Quran na Elimu nyengine..

      Huko Nyumbani Kuna watu wengi wanaoishi Nje wanataka kusaidia nyumbani lakini wanabanwa na kutotambuliwa.. Zanzibar sio kubwa ya Vijana kufika kuzurura.. Kuna watu wana ideas na miradi ya kimaendeleo lakini wanashindwa kuja kuwekeza nyumbani kutokana na Siasa Chafu na Majungu..

      Ikiwa raisi atafanya hayo aliowaihidi watu basi the future of zanzibar looking bright.. hii itawasaidia hata nduguzetu wa tanganyika wanaohamia Zanzibar na kuuza Karanga na vinyago..

      Delete
  22. Huu ujumbe, "ETI" tunataka kuwasaidia Wanzanzibar wanaoishi nje ambao watajiunga na hizo Diasporas zao na kama wanataka kuja kuwekeza

    Je wazanzibari wanaoishi nje ambao hawana uwezo wa kuja kuwekeza hawana haki ya kuwa wazanzibari?

    Watakuwa hawana haki ya hivyo vitambulisho?

    Nini maana ya kuwekeza?

    Kwani ni lazima mtu aje kuwekeza kwa mradi gani?

    Je wale Wazanzibari wanaocheza soka ambao wamekulia na kuzaliwa nje wanao uwezo wa kuja kuwekeza katika timu ya Taifa ya Zanzibar katika mashindano yoyote?

    Au kuwekeza ni kuuza makorokoro tu?

    Watu wanawekeza katika soka a mambo mengine leo mchezaji akitaka kurejea katika nchi yake aipe nguvu kama nchi zote duniani basi inaonekana kama ni dhambi,eti kwa sababu Nyerere alisema hakuna uraia wa nchi mbili.


    Diaspora ihakikishwe kwamba hawapewi vitambulisho vya kura kupitia mlango wa nyuma au ihakikishwe na Wazanzibar wote wanaoishi nje ya nchi wapewe haki kama hizo sawa

    Nnataka kuuliza Mzanzibari akitaka apewe hicho kitambulisho akija nyumbani asipate matatizo na hana haja ya visa mpaka ajiunge na diasporas?,

    Nnatoa tahadhari hivyo vitambulisho mwisho wake vitafikia kwa Wanigeria wakuleteeni unga hapo kwenu wakijua hawahitaji visa, wao watakuwa ni wazazi wao ni wazanzibar lakini wamezaliwa na kukulia Nigeria au sehemu njngine yoyote ile,

    Ukiamua kumpa mzanzibari kitambulisho kama hicho, kwanini iwe tu ni lazima mtu ajiingize katika siasa au vikundi vikundi , tafuteni kitu ambacho kitawalenga wazazibari wote walioko ndani na nje, mbona hao ndugu zetu huko nyumbani wao wagelishukuru zaidi kama wangelialikwa hio tonge hapo ikulu kuliko hao wenye uwezo wa tonge yao wanaoishi nje na chakula.

    Hapo ni lazima kuna changa la macho kama anavyosema mdau hapo juu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.