Habari za Punde

Taarifa ya CUF kwa umma na vyombo vya habari

Bila ya shaka kila mmoja wetu ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ameshtushwa kwa kiasi kikubwa baada ya kupata taarifa ya kunyanyaswa vikali pamoja na kufanyiwa matendo ya kulawitiwa viongozi wa Jumuia ya Uamsho Zanzibar.
 
Matendo haya katika hali ya kiubinadamu hayafai kabisa na nidhahir kwa kila mmoja wetu kuyapiga vita ili jamii na mataifa kwa ujumla wazisikie sauti zetu juu ya viongozi hawa wakubwa wa Dini ya Kiislamu.
 
Tukiwa kama taasisi kubwa ya hapa Tanzania Chama cha Wananchi CUF tunalaani vikali ukatili na ushenzi uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na wenzao 19.
 
Kwa mujibu wa walivyoeleza watuhumiwa hao wakiwa Mahakama ya kisutu Shekh Farid Had Ahmed na wenzake Jeshi la polisi limewafanyia ukatili wa hali ya juu usiostahili kwa binadamu.
 
Mahabusu hao wanaozuliwa huko Daresalam wanadai kuhojiwa wakiwa uchi wa mnyama, kulawitiwa na askari wa Jeshi la polisi, kuwekewa vitu vyenye ncha kali kwenye sehemu za haja kubwa na mateso mengine mengi ikiwa ni pamoja na kupigwa hadi kuumizwa.

Hata kama ni wakosaji matendo haya ni kinyume na haki za binadamu hayapaswi kufanyiwa binadamu kama hawa tena raia halali wa Nchi hii.
 
Tunauliza ipo wapi haki ya kisheria ya mwananchi wan chi hii ikiwa jeshi la polisi ndio wanaovunja sheria baada ya kulinda sheria?
 
Inashangaza kuona vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Makaburu dhidi ya Watu weusi wa Afrika Kusini sasa Vinafanywa na Vijana wa Kitanzania dhidi ya Watanzania wenzao kwa kisingizio cha Ugaidi.
 
Sisi CUF hatuoni mantiki ya uvunjaji wa Haki za Binadamu kwa kiasi hiki kwa watu wanaotuhumiwa kwa kile kinachoitwa kujishirikisha na Matendo ya Kigaidi.
 
Hata kama watuhumiwa hao watatiwa hatiani kwa makosa hayo, bado hukumu yao haitakua kulawitiwa kama ilivyoelezwa na mmoja kati ya Watuhumiwa hao mbele ya Mahakama.
 
Polisi mnapaswa kujua kwamba mnaowafanyia matendo hayo bado ni watuhumiwa tu wa matendo ya ugaidi je wakishinda kesi na kuonekana hawana hatia na nyinyi mchukuliwe hatua za kisheria?
 
Ikiwa matendo hayo yanafanywa kwa makusudi na Jeshi la Polisi dhidi ya Viongozi wa Dini ya kiislamu tena yenye asilimia 99 ya wakaazi wa Zanzibar hivi munataka wafuasi wao na Familia zao wafanye nini ?
 
CUF-Chama cha Wananchi kutokana na kauli mbiu yake ya ‘’haki sawa kwa wote’’ tunamtaka Rais kutoa kauli na Msimamo wa Serikali dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji huu uliofanywa na Jeshi la Polisi ili Wananchi wapate kujua hatua zitakazo chukuliwa na Serikali sambamba na kukubali Ombi la Watuhumiwa la kufanyiwa uchunguzi wa Afya zao kama lilivyo wasilishwa kwenye Mahakama inayosikiliza Kesi hiyo.
 
Tunatoa wito kwa Taasisi za kimataifa na kitaifa zinazoshughulikia mambo ya Uvunjwaji wa Haki za Binaadamu kufuatilia kwa Karibu suala hili na kuchukua hatua zinazostahili vingenevyo siku moja wanaweza kushuhudia maiti ikipelekwa mahakamani kama walivyodai watuhumiwa hao mbele ya Mahakama ya kisutu.
 
Tumeshuhudia malalamiko ya watuhumiwa hao kupitia vyombo vya habari wanasema kwamba mpaka hivi sasa wale waliojeruhiwa bado wanaugulia maumivu na hawajapewa matibabu yoyote yale licha ya kufanyia matendo makubwa ya kishenzi wanaendelea kusota ndani tu hivi hamuoni kama hii ni hatari zaidi kwa watuhumiwa hawa?
 
Tukiwa kama wadau wakubwa wa Chama cha siasa hapa Nchini tuna imani kwamba taarifa yetu hii itafanyiwa kazi na hatua za kisheria kuchukuliwa haraka sana iwezekanovyo ili kuepusha majanga zaidi ndania ya Nchi yetu.
 
Chama cha Wananachi CUF kinawaomba ndugu na jamaa pamoja na waislamu wote Nchini kuendelea kuwa na subra tukiamini kwamba sheria itachukuliwa dhidhi ya viongozi hawa.
 
Imetolewa na
 
Abdul Kambaya
 
Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi CUF.

1 comment:

  1. Mungu atawasaidia kama kweli wamefanyiwa ukatili huu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.