Na Kija Elias, Moshi
MKAZI mmoja wa eneo la Sabuko
kata ya Ibiriri wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kumbaka mtoto
mwenye umri wa miaka mitatu,na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za
siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani
Kilimanjaro, Koka Moita, amethibitisha kutokea tukio hilo na kumtaja mtuhumiwa
kuwa ni Emmanuelo John, ambaye ni mjomba wa mtoto huyo.
Alisema mtuhumiwa anadaiwa kufanyatukio
hilo Oktoba 8, mwaka huu majira ya saa 10:45 jioni katika eneo la Sabuko kata
ya Ibiriri, wilayani Siha mkoani hapa.
Alisema mama mzazi wa mtoto
huyo alimwacha mtoto wake nyumbani na mjomba wake huyo, huku yeye akienda
kujitafutia riziki na ndipo aliporejea alikumta mtoto huyo akiwa analia huku
akitokwa na damu sehemu za siri.
Alisema mtoto huyo kwa sasa
anapatiwa matibabu hspitali ya taifa ya Kibong’oto na kwamba mtuhumiwa
anaendelea kuhojiwa.
Alisema matukio ya ubakaji kwa
sasa yameendelea kuongezeka mkoani Kilimanjaro na hivyo, kuwataka wazazi kuwa
makini na watoto wao.

No comments:
Post a Comment