Na Amina Omari, Tanga
UAMUZI wa serikali kuchagua
teknolojia ya SMART CARD kutumika katika vitambulisho vinavyozalishwa na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) umeipa Tanzania sifa kubwa barani
Afrika.
Hayo yalibainishwa na
Mkurungezi wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari kutoka (NIDA), Joseph Makani,
wakati akisoma hotuba kwa niaba ya
Mkurungenzi Mkuu, wakati wa uzinduzi wa zoezi la usajili na utambuzi wa
watu mkoa wa Tanga.
Alisema hatua hiyo itasaidia
taifa na watu wake kuleta mabadiliko makubwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii
kutokana na kuwepo kumbukumbu za taarifa sahihi kuhusu hali zao.
Aliwaomba watendaji kuhakikisha
wanawajibika ipasavyo kuhakikisha zoezi la usajili na utambuzi kwa mkoa wa
Tanga, linafanikiwa kwa ufanisi.
Nae Mkuu wa mkoa wa Tanga, Chiku
Gallawa, aliwataka viongozi kuwapatia maelezo muhimu watendaji wa mitaa, vijiji
na kata kuhusu namna bora ya ujazaji wa fomu za vitambulisho.

No comments:
Post a Comment