Na Khamisuu Abdallah
MTOTO Shafik Shaisu Othman (10)
mkaazi wa Fuoni, amefariki dunia wakati akiogelea katika bwawa la kuogelea
liliopo katika bustani ya wanyama Zanzibar Park, wakati akisherekea sikukuu ya
Eid el Hajj.
Akizungumza na Zanzibar Leo
ofisini kwake Muembemadema, Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi, Mkadam
Khamis Mkadam, alisema tukio hilo lilitolea juzi saa 8:30 mchana na kusema kifo
chake kilitokana na kuzidiwa na maji.
Alisema polisi wanaendelea na
upelelezi ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Hivyo aliwataka wazazi
kusimamia watoto wao wanapokwenda katika sherehe mbalimbali hasa za sikukuu na
kuwashauri wamiliki wa bustani hiyo kuweka kima maalum cha maji kwa watoto na
watu wazima ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima.
Wakati huo huo Kamanda Mkadam
alisema tukio jengine lilitokea Oktoba 7 mwaka huu saa 11:00 jioni wakati Adam
Haji (22) mkaazi wa Magogoni alipofariki dunia wakati akiwa anafua.
Aidha alisema kifo cha marehemu
huyo kilisababishwa na saruji ya nyumbani kwao kupata maji iliyosababisha
kuteleza na kufariki dunia papo hapo.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha
kifo cha marehemu kilisababishwa na umeme.
Alisema mwili wa marehemu ulipelekwa
hospitali kuu ya Mmnazimmoja kwa uchunguzi na kukabidhiwa jamaa zake kwa
mazishi.

No comments:
Post a Comment