Na Zuhura Juma, Pemba
Mkuu wa Mkoa wa kaskazini
Pemba, Omar Khamis Othman, ameitaka Wizara ya Kilimo kuongeza bidii ya kuotesha
miche ya mikarafuu na kuigawa kwa wakulima.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Wete, alisema wananchi katika mkoa wake sasa wamehamasika
kupanda mikarafuu kwa wingi, ili kujipatia maendeleo.
Alisema kwa vile wananchi
wamehamasika na kilimo hicho, hakuna budi wizara kuongeza bidii ya kupanda
miche ili kuwahamasisha zaidi wakulima hao.
Alisema uchumi katika mkoa huo
umekua, kwani wananchi wamekubali kujituma katika njanja tofauti ikiwemo kilimo
kwa upanda mazao ya biashara na mbogamboga.
Akizungumzia amani na utulivu
katika mkoa wake, alisema inardhisha na kusema atahakikisha inadumishwa.
Let do business unusual, tuwafundishe wakulima wazalishe miche ya mikarafuu wenyewe badala ya kuwaachia Wizara ya Kilimo.
ReplyDelete