Na Khamisuu Abdallah
Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kimeipongeza serikali
kwa kuweka muundo mzuri wa utumishi
ambao umeonesha matumaini mema kwa walimu.
Akizungumza na vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa
chama hicho, Mussa Omar Tafurwa, alisema muundo huo umeridhiwa na walimu.
Alisema pamoja na kuuridhika na muundo huo
lakini wasiwasi wao upo katika utekelezaji hasa kwa walimu waliofanya kazi miaka
mingi.
Alisema ni vyema kuangaliwa vigezo sahihi vya
upandaji wa madaraja ili kuwepo usawa.
Alisema mwalimu yeyote atakaepata barua hiyo aiwasilishe
katika chama chao ili apate msaada.huo wa utumishi.
Akizungumzia siku ya walimu duniani, alisema kwa
mwaka huu maadhimisho ya siku hiyo yalishindwa kufanyika kutokana na
kuingiliana na skukuu ya Eid al Hajj.
Alisema kwa sasa walimu wameanza kuadhimisha
siku hiyo katika wilaya kwa kufanya mambo ya kijamii ikiwemo usafi wa mazingira
na makongamano ambapo kwa wilaya ya mjini yatafanyika wiki ijayo.
Alisema chama chao kimekubaliana sherehe hizo
zitakuwa zikifanyika kitaifa kila baada ya miaka mitatu ili kuwapa fursa walimu
wote kushiriki kikamilifu.
No comments:
Post a Comment