Habari za Punde

DW Akademie Yatoa Mafunzo Kwa Wafanyakazi wa ZBC

Mkufunzi wa Mafunzo ya Utayarishaji wa vipindi vya Mitaani kutoka DW AkadeMr. Charles Achaye-Odong, akitowa shukrani zake kwa washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kwa ukamilifu na kuandaa vipindi vya miataani kutokana na kupata uwezo wa kuandaa vipindi hivyo kupitia mafunzo hayo, kwa Wafanyakazi wa ZBC TV na ZBC Redio, yalioandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Vyombo vya Habari ya DW Akademie kanda ya Afrika Mashariki. tafrija hiyo imefanyika katika hoteli Pagoda Shangani Zanzibar.
Viongozi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar ZBC wakiwa katika hafla hiyo wakimsikiliza Mr Charles Achaye-Odong, akizungumza katika hafla hiyo, iliofanyika hoteli ya Pagoda Shangani Zanzibar.
                 Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika ukumbi wa mkutano
Washiriki wakipata msosi wa kichina katika hoteli ya pagoda shangani Zanzibar baada ya kupata kitabu cha utaalam kutoka kwa wakufunzi wa DW Akademie.
                         Mambo ya msosi wa kichina hayo full kujichana na bata

Mshiriki wa mafunzo hayo Mtangazaji Bi Hasina, akitowa shukrani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo baada ya kupata chakula kilichoandaliwa na DW Akademie, kwa washiriki hayo baada ya kumaliza mafunzo yao na kuahidi kuyatumia kwa kuandaa vipindi mbalimbali vya mitaani na kurushwa katika vituo hivyo.

Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya kuandaa vipindi vya mitaani ilioandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Vyombo vya Habari Afrika  DW Akademei, wakimsikiliza Muandaaji wa Mafunzo hayo East Afrika , Mr Charles Achaye-Odong, akizungumza na Viongozi na Washiriki wa mafunzo wakati wa hafla ya ufungaji iliofanyika katika hoteli ya Pagoda Shangani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.