STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 8.12.2014

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Mhe. Mkusa Issack Sepetu,
kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Wakati huo huo,
Dk. Shein amemuapisha Bibi Halima Maulid Salum, ambaye anakuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Miongoni mwa
viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif
Ali Idd, Dk. Mwinyihaji Makame Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala
Bora, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mhe. Haji
Omar Kheir na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
Wengine ni Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla
Mwinyi Khamis, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib
Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment