Na Husna Sheha
WANANCHI wa kijiji cha
Makunduchi wametakiwa kuendeleza mshikamano na kujiepusha na migogoro ili
kulibakisha eneo hilo kuanedelea kuwa kitovu na chemchem ya utulivu na elimu
kama ilivyokuwa zamani.
Wito huo ulitolewa jana na Mufti Mkuu wa
Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi, wakati akizungumza na baadhi ya wazee wa
kijiji hicho katika ukumbi wa afya Makunduchi wilaya kusini Unguja.
Aidha aliwakumbisha wazee hao
juu ya historia isiyofutika ya kijiji hicho kuwa chimbuko la masheikh wakubwa wa Zanzibar kama
vile Sheikh Hassan Bin Ameir, Sheikh Fatawi Bin Issa na Sheikh Ameir Bin Tajo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Mufti,Sheikh Fadhil Soraga,
ziara hiyo ya Mufti ni mfululizo wa ziara zake kutembelea wilaya zote za Unguja
na Pemba .
Katika ziara hiyo alifuatana na
maofisa mbali mbali wa ofisi yake pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa
la GNRC, Sheikh Abubakar Francis Babuogi.
No comments:
Post a Comment