Na Laylat Khalfan
Ofisa Mteule wa daraja la kwanza
wa dawati la jinsia na watoto la polisi,Sajenti Zahor Faki Mjaka, amesema
kumezuka mtandao wa ukahaba ambao wahusika huwapigia simu wanawake kutoka
maeneo mbali mbali wakiwataka waje Zanzibar kufanya kazi za ndani, lakini baada
ya kufika wanawalazimisha kufanya ukahaba.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi ofisa kwake Madema, alizitaja miongoni mwa nchi ambazo wasichana
hao wanatoka kuwa ni Tanzania Bara, Kenya, Uganda na nchi nyengine jirani.
Alisema vitendo hivyo hufanywa
na baadhi ya mawakala wasio waaaminifu.
Alisema mawakala wanaojihusisha
kwenda mtandao huo wamekuwa wakijificha kiasi ambacho si rahisi kuwagundua.
Alisema tabia hiyo imeshamiri
zaidi katika mtaa wa Mjimkongwe.
Alisema polisi wanafanya
jitihada kuwabaini na kuwakamata watu hao ili kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Kwa kweli hao watu hatujawabaini kwani
inaonekana wanafanya vitendo hivi kwa kujificha kiasi ambacho huwezi kuwagundua
mara moja,”alisema.
Akizungumzia kuhusu vitendo vya
udhalilishaji kuongezeka, alisema ni kutokana na jamii kukosa ushirikiano wa
pamoja.
Alitoa wito kwa jamii kutoa ushirikano
wa dhati wanapoona vitendo kama hivyo vinafanyika katika mitaa yao ili kusaidia
kuvidhibiti.
Alisema jina la mtandao huo
unajulikana kama “help me” kwa wanawake na wanaume unajuillikana “Iga ufe”.
No comments:
Post a Comment