Na Mwanajuma Abdi, DAR ES
SALAA
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkesha
Mkubwa wa Kitaifa, Mchungaji wa kanisa la Tanzania Fellowship, Godfrey Malassy,
amesema amani ya Tanzania ipo kama ‘yai’, ambalo likivunjia haliwezi kurudishwa
tena, hivyo aliwahusia baadhi ya wanasiasa kuacha kutumia lugha za uchochezi,
za kuvuruga na kuhataraisha utulivu nchini.
Hayo aliyasema jana, wakati
akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa habari Maelezo, kuelezea dua
maalum ya kitaifa itakayofanyika mkesha wa maka mpya Disemba 31, ambayo
itahusisha mikoa 16 ya Tanzania, ambapo kwa Dar es Salaam itafanyika uwanja wa
taifa na Zanzibar utafanyika uwanja wa Amaan.
Alisema amani ya Tanzania
imebarikiwa na Mwenyezi Mungu, hivyo wanasiasa na wananchi wanatakiwa kuienzi,
kuidumisha na kuilinda badala ya kutoa lugha za umwagaji damu ambazo zinaweza
kuliingiza taifa katika matatizo makubwa.
Kauli mbiu katika mkesha huo ni
‘itunze, ilinde,ihubiri amani ya nchi yako’, ambapo alitoa wito kwa Watanzania kutochezea
amani kwani ikipotea hawataweza kuirejesha tena, hivyo kuna kila sababu ya
kuliinda.
Alisema mkesha huo
umewashirikisha waimbaji wa kwaya kutoka madhehebu mbali mbali ili nchi iweze
kuombewa amani kwa kumaliza mwaka kwa usalama na kuukaribisha mwaka mpya.
Alisema kuombea dua taifa haihusishi dini fulani hivyo
alitoa wito kwa waumini wa dini nyengine kuungana nao pamoja katika kuliombea taifa.
Akitoa mfano wa Zanzibar kuna Waislamu
zaidi ya asilimia 99 lakini mkesha huo unafanyika katika uwanja wa Amaan,
ambapo wakaazi wa huko wameipokea vizuri dua hiyo, hivyo kuna kila sababu ya
watu kuungana na kushirikiana ili kuombea nchi.
Alisema baadhi ya nchi za Afrika
zinalia kila siku kutokana na kukosekana amani, wanashindwa kulima vizuri
pamoja na shughuli za kimaendeleo akitoa mfano nchi ya Congo na kwengineko
ambako utulivu umekosekana.
No comments:
Post a Comment