Habari za Punde

Notisi ya Kuwashitaki Waajiri Mbalimbali Zanzibar.

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR
NOTISI YA KUWASHITAKI WAAJIRI MBALIMBALI


 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) unatoa taarifa kwa umma kwamba utawachukulia hatua za kisheria za kuwashitaki Mahakamani waajiri mbalimbali waliotajwa katika notisi hii kwa kosa la kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar kinyume na kifungu cha 17(1) (2) na (3) cha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, Sheria Na.2 ya mwaka 2005 na kwa vipindi tofauti. Waajiri ambao watafunguliwa mashtaka ni hawa wafuatao:-
1    1      RAMAYN INTERNATIONAL SCHOOL – KWA MCHINA ZANZIBAR                                   
2.       D.B SHAPRIYA &CO.LTD – HANYEGWA MCHANA ZANZIBAR
3.       THE FLOATING RESTAURANT – FORODHANI ZANZIBAR
4.       HOTEL INTERNATIONAL – MCHAMBA WIMA ZANZIBAR
5.       FUMBA BEACH LODGE – FUMBA ZANZIBAR
6.       MERCURY RESTAURANT – MALINDI ZANZIBAR
7.       MOMBASA CENTRAL – KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR
8.       THE NUNGWI INN- NUNGWI ZANZIBAR
9.       SUFA PRIMARY AND SECONDARY SCHOOL- MAGOMENI MPENDAE
10.   HOTEL EXECUTIVE COMPANY LTD- KILIMANI
11.   ALL NATION ACADEMY – KISAUNI ZANZIBAR
12.   MWANANCHI ENGINEERING AND CONTRACTING COMPANY LTD
13.   TATU LTD- SHANGANI ZANZIBAR
14.   MALIK FARAJ – AMANI ZANZIBAR
15.   BARZANGY INC LTD- MIGOMBANI
16.   MASS GLOBAL INVESTMENT LTD – MPIRANI ZANZIBAR
17.   SHU LTD – FORODHANI ZANZIBAR
18.   RIALMA COMPANY LTD- MICHAMVI ZANZIBAR
19.   ISLAND SECURITY & GENERAL CLEANERS CO. LIMITED –KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR
20.   SERENITY DEVELOPMENTS LTD/AL JOHAR – SHANGANI ZANZIBAR
21.   TAALIM COMPUTER CENTRE – MACHOMANE PEMBA
22.   IMARA TOURES – CHAKE CHAKE PEMBA
23.   SWAHILI DIVERS – MAKANGALE PEMBA
24.   VILA DIDA – PWANI MCHANGANI ZANZIBAR

Hivyo basi, Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar unawataka wamiliki, waendeshaji au wahusika wa taasisi hizi kulipa madeni ya michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Hifadhi ya jamii Zanzibar si zaidi ya siku saba (7) kutoka tarehe ya  notisi hii na kushindwa kufanya hivyo Mfuko utawafungulia mashitaka dhidi yao.

IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MWENDESHAJI
MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR.

‘ZSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE

1 comment:

  1. Hongera kwa hatua hiyo, lakini pia kuna taasisi nyingi hasa za binafsi zisizofuata taratibu sahihi za uajiri. Mahoteli mengi yanaajiri wafanyakazi bila ya hata mikataba na ukijaribu kusema ndo huna kibarua tena. Naomba na hili nalo lichukuliwe hatua.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.