Habari za Punde

Katibu Mkuu Atowa Mkono wa Pole kwa Ndugu wa Marehemu Issa Ahmeid Kijiji kwao Kisiwani Pemba akiwa katika ziara yake.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa CCM na wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa nyumbani alipozaliwa marehemu Issa Ahmed Othman Mshauri wa Rais Zanzibar katika masuala ya Utalii,aliyefariki nchini India alipoenda kwa matibabu,Katibu Mkuu alitoa salaam za pole kwa familia ya marehemu na ndugu zake kupokelewa na kaka wa marehemu Othman Ahmed Othman (katikati) na anayefuati ni Waziri Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Mohammed na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, walipofika nyumbani kwao Shenge Juu,Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa CCM na wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  wakiwa nyumbani alipozaliwa marehemu Issa AhmedOthman,Shenge Juu Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiondoka nyumbani alipozaliwa marehemu Issa Ahmed Othman baada ya kutoa pole kwa kaka wa marehemu Othman Ahmed Othman, Shenge Juu Pemba ,tarehe 25 Januari 2015.

3 comments:

  1. Taarifa iliyopita umesema kazaliwa pandani,wete.hapa unatuambia kazaliwa shenge juu.
    Be serious na kazi ndugu

    ReplyDelete
  2. Hajakosea Pandani ni jimbo la shengejuu.

    ReplyDelete
  3. Kuna jimbo linaitwa shengejuu?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.