MKURUGENZI Mtendaji wa Umoja wa watu
wenye ulemavu UWZ, Zanzibar Rashid Ali Mohamed akielezea azma ya mradi wa kupinga
udhalilishaji wa kijinsia, hasa kwa watu wenye ulemavu wa akili, kwenye mafunzo
yaliofanyika ukumbi wa ZANZGOC Micheweni Pemba, kulia ni Msaidizi Naibu Katibu
mkuu wa UWZ, Salim Abdalla Salim na katikati ni Afisa tawala wilaya ya
Micheweni Ahmed Khalid, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
AFISA Mipango wa kituo cha huduma za
sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalifan Amour Mohamed akitoa mada juu ya
vikwazo vilivyopo, katika kumaliza kesi za udhalilishaji wa kijinsia, kwenye
mafunzo yaliondaliwa na UWZ yaliofanyika Micheweni, katikati ni sheha wa shehia
ya Micheweni Dawa Juma Mshindo na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa
watu wenye ulemavu UWZ, Zanzibar Rashid Ali Mohamed, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WASHIRIKI wa mafunzo ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia
hasa kwa watu wenye ulemavu wa akili yaliofanyika Micheweni na kuandaliwa na
UWZ kwa kushirikiana na ZLSC na ZAFELA , (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
HAKIMU wa mahakama ya mkoa Chake Chake,
Khamis Ali Simai akichangia maoni yake, kwenye mafunzo ya kupinga udhalilishaji
wa kijinsia hasa kwa watu wenye ulemavu wa akili, yalioandaliwa na UWZ na
kufanyika Micheweni Pemba, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment