Habari za Punde

Resi za Ngalawa Kusherehekea Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdilah Jihad, akisalimiana na manahodha wa ngalawa zinazoshiriki resi za ngalawa yaliofanyika katika ufukwe wa pwani ya forodhamchanga Zanzibar. 
Ngalawa zinazoshiriki resi za ngalawa zikiwa katika matayarisho ya kuaza resi hizo.Jumla ya ngalawa 10 zimeshiriki resi hizo zilizofanyika katika ufukwe wa foromchanga. 
Ngalawa zinazoshiriki resi za ngalawa zikiwa katika matayarisho ya kuaza resi hizo.Jumla ya ngalawa 10 zimeshiriki resi hizo zilizofanyika katika ufukwe wa foromchanga. 
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Zanzibar Mhe.Abdilah Jihad, akiazisha resi za Ngalawa katika ufukwe wa pwani ya forodhani ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika resi hizo nafasi za mwanzo zimechukuliwa na ngalawa za njia namba 7 Dimani, Nyamazi na Fumba Unguja.
Mambo yameaza baada ya kuazishwa kwa resi hizo na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdilah Jihadi kuamuru kuaza resi hizo.
Ngalawa zikichomoka kuaza resi hizo kwenda kuzunguka kisiwa cha jirani na ufukwe huo kulikowekwa boya. 


Wananchi waliofika katika ufukwe wa pwani wa forodhani wakiangalia resi za ngarawa zikiaza katika ufukwe wa pwani ya forodhani.

Waasisi wa Resi za Ngalawa katika miaka ya 1976, wakifuatilia michezo hiyo wakikumbua enzi zao walivyokuwa wakishiriki resi za ngalawa na kuzikutanisha Ngalawa za Kizingo, Bumbwini Dimani na nyeginezo wakati huo kulikuwa na upinzani mkubwa.ngalawa za kizingo na bumbwini.
Ngalawa ya Dimani inayoitwa Kindumbwendumbwe inayoongozwa na Nahodha Ndg Abuu Hassan Kondo ikiingia ikiwa mshindi wa kwanza wa resi za Ngarawa zilizofanyika katika ufukwe wa pwani ya Forodhani jumla ya ngarawa kumi zimeshiriki mashindano hayo.
Washindi wa Pili na Tatu wakimalizia mashindano hayo ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika katika ufukwe wa pwani ya forodhani Zanzibar , Mshindi wa Pili Ngarawa ya inayoitwa Dokta ya Dimani Unguja na ya Tatu Mbaya Hawekwi zote za Dimani Unguja.
Wananchi wapenzi wa mchezo wa resi za ngarawa kutoka sehemu mbalimbali za Unguja wakifuatilia resi za ngarawa zilizofanyika katika ufukwe wa pwani ya forodhani Unguja na kushirikisha ngarawa kumi kutoka Unguja Kindumbwendumbwi ya Nyamanzi, Dokta ya Dimani, Mbaya Hawekwi ya Bumbwini, Kesho Tena Nyamazi Edd-Mubaraka ya Bumbwini Amantul Lilah ya Bumbwini.
Wapenzi wa mchezo wa resi za ngalawa wakiwa katikac ufukwe wa pwani ya forodhani wakishuhudia resi hizo.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe Abdillah Jihad, akimkabidhi zawadi yake mshimdi wa kwanza wa Resin a Ngarwala Nahodha wa Ngarawa Kindumbwendumbwe ya Nyamazi Ndg Abuu Hassan Kondo baada kushika nafasi ya kwanza katika resi hizo za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika ufukwe wa pwani ya forodhani


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.