Habari za Punde

Walimu kutoka kiruna Sweden wawasili nchini

Walimu 18 kutoka Kiruna, Sweden wawasili leo kwa ajili ya kuanza kazi ya ufundishaji. Walimu hao watakaokuwa nchini kwa kipindi cha mienzi minne watasomesha ujasiriamali, kiingereza, kompyuta na demokrasia kwa watoto wa kike wa Makunduchi. Kuja kwao nchini kunafuatia makubaliano baina ya wadi za Makunduchi na Manispaa ya Kiruna. Ujumbe wa wadi za Makunduchi ulifanya ziara ya kikazi ya wiki moja mwanzoni mwa Disemba mwaka jana.

Walimu wa Kiruna, Sweden wapokelewa kwa shangwe na wanafunzi na wazee wa Makunduchi kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar

Afisa tawala mstaafu wa wilaya ya Kusini, ndugu Abdallah Ali Kombo akionekana kuwa na furaha wakati akimpokea ndugu Simon, mmoja ya walimu watakaofundisha watoto wa kike huko Makunduchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.