Na Tausi Ally
Kesi ya ugaidi inayowakabili viongozi 23 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu sasa kusikilizwa na Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda.
Awali kesi hiyo ambayo itatajwa Januari 13,2015 kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa ambaye hata hivyo alijitoa.
Ni baada ya wakili wa washtakiwa hao wa ugaidi, Abubakar Salim kumtaka ajitoe kuisikiliza kesi hiyo ili iweze kupangiwa hakimu mwingine ambaye atatoa uamuzi juu ya hoja zao walizozitoa mahakamani hapo Septemba 19,2014.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ya ugaidi ni Sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mbuyuni Zanzibar, Fundi Ujenzi mkazi wa Koani Zanzibar, Noorid Swalehe na Jamal Nooridin Swalehe (38).
Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.
Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu kwa pamoja wanadaiwa kuwa walijihusisha na makosa hayo ya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi ya 2002.
Wanadai kuwa kati ya mwezi Januari 2013 na Juni 2014 walipanga njama ya kutenda makosa hayo ya kula njama za kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo vya kigaidi.
Katika kipindi hicho na maeneo tofauti nchini, Sheikh Farid na Sheikh Mselem Mselem wanadaiwa kuwaingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.
Sheikh Farid anadaiwa kuwa kwa makusudi na akijua alitoa msaada kwa watu hao wa kutenda vitendo vya kigaidi kinyume cha sheria na kuwahifadhi.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment