Meneja wa Shamba la Chuo cha Kilimo Kizimbani liliopo Makurunge Magamoyo Nd. Abdulrahman Mahmoud Hamid akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa ziara yake ya kulikagua shamba la SMZ waliokabidhiwa chuo hicho.
Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi Zanzib ar Mh.Abdulla Shaaban, Waziri wa Kilimo Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwamboyta na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nd. Ali Khalil Mirza.
Balozi Seif akitafakari na Mwanasheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa SMZ Bwana Saleh Said Mbarouk akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kulia yake Nd. Hemed Mwanga mwenye miwani, Waziri wa Kilimo Bara Mh. Steven Wasira na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Baadhi ya sehemu ya shamba la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar liliopo Makurunge Bagamoyo ambalo limekabidhiwa Chuo cha Kilimo Kizimbani ili kuliendeleza.
Ujumbe wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar uliotembelea shamba la Mifugo la SMZ la Makurunge waliangalia fukwe ya Bagamoyo iliyomo pembezoni mwa shamba hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kati kati na ujumbne wake wakifurahia fukwe safi iliyomo ndani ya shamba la Serikaliu ya Mapinduzi ya Zanzibar liliopo Makurunge.Kushoto ya Balozi Seif ni Meneja wa Shamba hilo Nd. Abdulrahman Hamid Mahmoud, wakati kulia ya Balozi Seif ni Katibvu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Nd. Afan Othman Maalim, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Kilimo Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwambioya na Naibu Waziri wa ARDHI Bara Mh. Angela Kairuki.
Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Tanzania Bara Mh. Angela Kairuki akimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Wizara hiyo itasimamia kukamilisha taratibu zote zitakazothibitisha uhalali wa umiliki wa SMZ katika shamba la mifugo la Makurunge Bagamoyo Mkoa wa Pwani.Kulia ya Naibu Waziri wa Ardhi Mh. Angela Kairuki ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo(Picha na Hassan Issa OMPR)
No comments:
Post a Comment