Habari za Punde

Mafunzo ya Wadadisi wa Sensa ya Viwanda Yafunguliwa Dar leo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi 200 wa Sensa ya Viwanda itayofanyika nchi nzima  mwezi huu. Mafunzo hayo yanafanyika chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.
 .Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam Prof.Ngalinda Innocent akizungumza na wadadisi watakaokusanya takwimu za Sensa ya Viwanda mwezi huu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 14.
Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Ngalinda Innocent akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Maria Bilia (katikati) na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makzi Bi. Hajjat Amina Mrsiho Said leo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukusanya takwimu sahihi wakati wa Sensa ya Viwanda leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Bw.Hussein Kamote akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi 200  watakaokusanya takwimu wakati wa  Sensa ya viwanda itakayofanyika nchini mwezi huu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya NBS na wadadisi wa Sensa ya Viwanda.(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.