Habari za Punde

Michezo ya kuadhimisha miaka 38 ya JKU yazidi kupamba moto

Na Mwajuma Juma
 
MICHUANO ya kanda ya kusherehekea miaka 38 ya kuzaliwa kwa JKU Zanzibar inazidi kupamba kasi ambapo juzi kulifanyika michezo ya Mpira wa Mikono na Netiboli katika uwanja wa Saateni uliopo ndani ya kambi ya Jeshi hilo mjini hapa.
 
Katika mchezo wa mpira wa Mikono waandaji wa michuano hiyo JKU iliwafunga KMKM mabao 24-23 huku mfungaji ambae aliongoza kwa kufunga magoli kwa upande wa JKU alikuwa ni Mohammed Saleh aliefunga magoli manane akifatiwa na Rajab Ali aliefunga magoli matano.
 
Kwaupande wa KMKM mfungaji wao aliefunga magoli mengi ni Amour Said ambae alifunga magoli sita na Shaban Juma aliefunga magoli matano.
 
Kwa mchezo wa Netiboli ambao uliwashirikisha wa akinadada na kuwakutanisha JKU Veteran na Chipkizi ulimalizika kwa Veteran kushinda mabao 33-31.
 
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani JKU Veteran ilionesha umahiri wake wa mchezo huo huku Pili Peter (GS) akipachika magoli 23 kati ya 33 na mabao 10 yakifungwa na Siamini Ali (GA) na kwa Chipkizi mabao yake yalipachikwa na Dawa Mohammed (GS) aliyefunga magoli 16 na 15 yakifungwa na Mariam Rashid (GA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.