Habari za Punde

KMKM na Polisi uwanjani michezo ya marudiano

Na Mwajuma Juma, Zanzibar
WAWAKILISHI wa Zanzibar katika kombe la Klabu Bingwa Afrika KMKM wanashuka dimbani  kuumana na Elhilal ya Sudan kwa mchezo wao wa marudiano utakaochezwa uwanja wa Amaan sa 10:00 za jioni.
 
Mbali na KMKM kushuka kesho  lakini kwa upande wa Polisi ambayo inashiriki kombe la Shirikisho itacheza keshokutwa (Jumapili) na SC Muonana ya Gabon ambayo nayo ikicheza katika uwanja huo wa Amaan.
 
Itakumbukwa kuwa timu za Zanzibar katika michezo yao awali wakiwa ugenini wote walifungwa ambapo KMKM ilifungwa mabao 2-0 na Polisi ikafungwa mabao 5-0.
 
Kiujumla timu zote hizo ili ziweze kusonga mbele zinahitaji kila moja kushinda ambapo KMKM itahitaji ushindi wa mabao 3-0 na Polisi mabao 6-0.
 
Katika michezo yote hiyo viingilio vitakuwa ni shilingi 5000 kwa VIP, 3000 Wings na 2000 kwa majukwaa ya kawaida

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.