Habari za Punde

Skuli ya Kusini kuimarisha uhusiano na Skuli ya Sundsvall Gymnasium

Skuli ya Kusini impokea rafiki zao leo wanafunzi wapatao 11 na walimu wao 3 kutoka  Skuli ya Sundsvall Gymnasium nchini Sweden. Lengo la safari hiyo ni kuimarisha uhusiano uliokuwepo kati ya skuli hizo mbili ambazo hutembeleana kila mwaka. Wanafunzi wapatao 5 na walimu wao 3 kutoka Skuli ya Kusini wanategemewa kuondoka kwenda Sweden mwezi wa April mwaka huu. Katika picha mwalimu mkuu wa skuli ya Sundsvall ndugu Sweden akisalimiana na mwalimu wa skuli ya Kusini mara baada ya kuwasili uwanja wa kimataifa wa Zanzibar
                                   Wanafunzi wa Skuli ya Kusini wakiwasaidia wenzao kutoka Sweden
Picha ya pamoja ya walimu na wanafunzi wa skuli ya Kusini na Sundsvall Gymnasium kutoka Sweden kabla wageni hao hawajaelekea Makunduchi smbako wajifunza mambo mbali mbali ya utamaduni na taaluma pia. Aidha wanafunzi hawa kutoka Sweden watatoa msaada wa simu kwa wanawake wa shehia ya Tasani na Mzuri kaja. Msaada huo utawafikia pia kinamama walioshiriki kwenye Tamasha la Chakula cha asili ya Makunduchi ambalo litafanyika tena mwezi wa Agosti mwaka huu.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.