Habari za Punde

Balozi Seif Atembelea Nyumba ya Sheha wa Kibweni Ilioungua kwa Moto

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifajiri Familia ya Sheha wa Shehia wa Kibweni Bibi Asha Ali Nassor ambayo moja ya chumba cha nyumba hiyo kimeteketea na kuunguza vitu vyote vilivyokuwemo.kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Mohammed Mahmoud.
 Balozi Seif akikagua hasara iliyotokana na moto katika chumba cha Nyumba ya Sheha wa Kibweni Bibi Asha Ali Nassor Wilaya na Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi.kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Moh’d Mahmoud na kulia ya Balozi Seif ni Mmoja wa miongoni mwa wakaazi wa Nyumba hiyo Bwana Abdulla Kombo Hamad
Mtoto wa Sheha wa Shehia ya Kibweni anayeishi ndani ya chumba kilichoteketea kwa Moto Bibi Asumini Moh’d Juma akimueleza Balozi Seif mkasa ulimpata kutokana na maafa hayo ya moto.
.(Picha na Hassan Issa OMPR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.