Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akisalimiana na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Property International Abdulhalim Zahran, alipowasili Hoteli ya Hyatt Regency Dar es salaam kwa ajili ya kuzindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” na Jarida linalotolewa kila wiki Property International Magazine.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akihutubia Viongozi na watendaji wa kampuni ya Property International inayomilikiwa na watanzania wanaoishi Nchini Dubai wakati wa uzinduzi rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” na Jarida linalotolewa kila wiki Property International Magazine, uzinduzi huo umefanyika jana katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Property International LTD Mr. Mohammed Sharif baada ya kuzindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akisalimiana na watoto Cisco Nickson na Nasra Said alipokutana nao kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro wakati wa mapokezi ya Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akiwa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alipowasili katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa Kamati ya Ushauri ya Chama cha Kikomunisti cha China Mhe. Wang Jiarwi walipokutana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Ngur-doto jijini Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal, akiwa na Makamu wa Rais wa Kamati ya Ushauri ya Chama cha Kikomunisti cha China Mhe. Wang Jiarwi walipokutana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Ngur-doto jijini Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Kamati ya Ushauri ya Chama cha Kikomunisti cha China Mhe. Wang Jiarwi nje ya ukumbi wa Hoteli ya Ngur-doto jijini Arusha jana. (Picha na OMR)
No comments:
Post a Comment