Habari za Punde

PBZ Yakamidhi msaada kwa Wananchi wa Kwamtipura waliopata maafa ya Upepo na Mvua

Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Seif Suleiman akizungumza na Sheha wa Kwamtipura Ndg Machano Salum Khamis, alipofika katika shehia hiyo kukabidhi msaada wa mabati na miti kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya kuezuliwa mapaa ya nyumba zao na upepo na mvua za masika hivi karibuni.Jumla ya nyumba kumi na moja zimepata maafa hayo na kuwafanya wanafamilia kuwa katika mazingira maguu, 

Kaimu Mkurugenzi Masoko wa PBZ Ndg Seif Suleiman akikabidhi mabati kwa Sheha wa Shehia ya Kwamtipura na wananchi waliopata madhara hayo ya upepo, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya Kilimahewa Zanzibar.
 Kaimu Mkurugenzi Masoko wa PBZ Ndg Seif Suleiman akikabidhi mabati kwa Sheha wa Shehia ya Kwamtipura na wananchi waliopata madhara hayo ya upepo, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya Kilimahewa Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa PBZ Ndg Seif Suleiman akikabidhi mati Sheha wa Shehia ya Kwamtipura na wananchi waliopata madhara hayo ya upepo, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya Kilimahewa Zanzibar.


Kaimu Mkurugenzi Masoko wa PBZ Ndg Seif Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakati wa hafla ya kukabidhi mabati kwa wananchi wa Shehia ya Kwamtipura waliopata majanga ya upepo kuezua baadhi ya nyumba katika shehia hiyo na kuwataka wananchi hao kuwa na subira kwa mkasa huo na kutowa wito PBZ iko pamoja nao na imeguswa na hali hiyo kwa ajamii na kutowa msaada huo ikiwa ni moja ya kusaidia jamii katika maafa. 
Mkaazi wa kwamtipura Mjumbe wa Sheha Bi.Mwanajuma Aruba akitowa shukrani kwa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa msaada huo kwa wananchi wa shehia hiyo. na kuitaka hii isiyo mwisho kusaidia wananchi katika majanga mbalimbali na kuzitaka Taasisi nyegine kuchukua mfano wa PBZ kuwajali wananchi wanapofikwa na majanga.  



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.