Habari za Punde

Kinana atikisa Arusha mjini

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Arusha mjini kwenye uwanja wa mkutano wa Sheikh Amri Abeid ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM itaendelea kuwatetea watu masikini na itahakikisha inawapa nafasi za uongozi watu wanaokubalika na wananchi.
 Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Onesmo Ole Nangole akihutubia wananchi wa Arusha ambapo aliwataka mawaziri kufanya ziara vijijini badala ya kukaa maofisini.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Arusha mjini na kuwaambia pesa isitumike kununulia madaraka .

 Amani Ole Silanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli na kujiunga na CCM akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.



  Amani Ole Silanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli na kujiunga na CCM akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo alisema Chadema hakina watu wenye sifa za kuongoza.
 Aliyekuwa Mwenezi wa Chadema kata ya Olorien  Prosper Mfinanga (kulia) akionyesha baadhi mabango kwa Katibu wa NEC Itikadi wa CCM Taifa Nape Nnauye, Mwenezi huyo wa Chadema amejiunga rasmi na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimia wananchi kabla ya kuanza kuhutubia wananchi,
 Prosper Mfinanga aliyekuwa Mwenezi wa Chadema wilaya ya Olorien akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kujiunga na CCM.
 Wananchi wakifuatilia mkutano
 Waandishi wa habari wakihakikisha wanapata kila tukio
 Umati wa watu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Sheikh Amri Abeid tayari kuhutubia.












































Mwenyekiti wa Vijana wa CCM mkoa wa Arusha Robinson Meitinyiku akihutubia wananchi wa mkoa wa Arusha ambapo aliwaambia wananchi hao Kikwete amerahisisha miundo mbinu, ameongeza vyuo na shule za sekondari na za msingi ,ameboresha huduma ya afya ikiwa ndio tafsiri ya maisha bora kwa kila mtanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.