Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Wanawake wa Umoja wa Wawanawakw Wakikristo Waadhimisha kwa Ibada Zanzibar.

Baba Askofu Augustino Shao akiongoza Ibada ya kuitakia Amani Dunia wakati wa Maadhimishi ya Siku ya Wanawake, iliowajumuisha Wanawake wa Umoja wa Wawanawake wa Kikristo Zanzibar, Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Kikatoliki Minara mowili Zanzibar, na kuwashirikisha Wanawake wa madhehebu mbalimbali ya Dini ya Kikristo Zanzibar.  
 Waumini wa Kikristo Zanzibar wa Umoja wa Wanawake wa Kikristo wakiwa katika Ibada ya Amani kuitakia Amani Dunia na Tanzania katika kipiondi hichi cha kura ya maoni na Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu. 
 Masista wakijumuiya na Wanawake wa Umoja wa Wawanawake wa Kikristo Zanzibar wakifuatilia Ibada ya Maombi ya Amani Duniani huadhimishwa kilia mwaka. Ibada hiyo ilioongozwa na Askofu Baba Augustino Shao iliofanyika katika Kanisa la Minara miwili Zanzibar ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake.
Mmoja wa Mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kikristo Zanzibar akisoma maombezi ya kutakia Amani ikiwa ni siku ya Maombi Dunia wakiungana na Wakristo Duniani kuadhimisha siku hiyo kuitakia Amani Dunia.Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la Minara Miwili Zanzibar

Baba Askofu Augustino Shao na Paroko Cosmas Shayo, wakiwa katika maombi ya Amani Duniani ilioadhimishwa na Umoja wa Wanawake wa Kikristo Zanzibar.kwa kuaza kwa maandamano yalioazia katika viwanja vya maisara na kumalizikia katika viwanja vya kanisa la minara miwili shangani Zanzibar na kuendelea na Ibada hiyo ya Maombi.
                   Waumini wakiwa kanisani katika Ibada ya Maombi ya Amani Duniani.

Muumini akiombea Amani wakati wa Ibada ya Maombi ya Amani Duniani Maombi hayo yamefanyika katika Kanisa la Minara miwili Zanzibar na kuwajumuisha Wanawake wa Kikristo wa madhehebu yote Zanzibar 




                                       Waumini wakitakiana Amani wakati wa Ibada hiyo

                                         Waumini wakitakiana Amani wakati wa Ibada hiyo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.