UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU
LA WAPIGA KURA KATIKA KATA TISA (9) ZA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imeanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura baada ya kukamilika kwa maandalizi muhimu ya Uboreshaji wa Daftari,
ikiwemo manunuzi ya vifaa na upatikanaji wa fedha kutoka Serikalini.
Zoezi
la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, tofauti na Uboreshaji wa
Daftari hilo kwa Awamu zote za Chaguzi zilizopita, linafanyika kwa kutumia
teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR). Zoezi la Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilianza kufanyika katika Kata tisa (9) za
Halmashauri ya Mji wa Makambako katika Vituo 54 vilivyowekwa katika Mitaa na
Vitongoji, kuanzia tarehe 23/2/2015 katika Kata za Kitisi, Kivavi, Lyamkena,
Maguvani, Majengo, Makambako, Mji Mwema, Mlowa na Mwembetogwa.
Tume
ililenga kuandikisha Wapiga Kura 32,370 kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya
Takwimu za Sensa ya Idadi ya watu ya mwaka 2012. Tume ililenga kuandikisha kwa siku jumla ya
watu 1,850.
Hata hivyo mara baada ya uandikishaji kuanza idadi ya Wapiga Kura
waliokuwa wanajitokeza iliendelea kuwa kubwa na kuongezeka kila siku ambapo
kulikuwa na misururu mirefu ya watu waliojitokeza kujiandisha katika Vituo
vyote vya Uandikishaji. Tume ilivuka malengo yaliyowekwa ya Uandikishaji
kutokana na kujitokeza kwa wingi kwa Wapiga Kura waliofika katika Vituo vya
Uandikishaji kila siku kwa Kata zote tisa (9) za Mji wa Makambako ambazo
zilikuwa zinaandikisha Wapiga Kura.
Idadi
ya Wapiga Kura waliojitokeza na kuandikishwa kwa kila siku katika Kata tisa (9)
za Mji wa Makambako ilikuwa kama ifuatavyo:-
i.
Tarehe 23/2/2015 Tume
iliandikisha Wapiga Kura 3,014;
ii.
Tarehe 24/2/2015 Tume
iliandikisha Wapiga Kura 4,727;
iii.
Tarehe 25/2/2015 Tume
iliandikisha Wapiga Kura 5,301;
iv.
Tarehe 26/2/2015 Tume
iliandikisha Wapiga Kura 6,354;
v.
Tarehe 27/2/2015 Tume
iliandikisha Wapiga Kura 6,731;
vi.
Tarehe 28/2/2015 Tume
iliandikisha Wapiga Kura 6,545;
vii.
Tarehe 1/3/2015 Tume iliandikisha
Wapiga Kura 6,906;
viii.
Tarehe 2/3/2015 kutokana na Watu
waliokuwa wanajitokeza kujiandikisha kuendelea kupungua, Tume iliandikisha
Wapiga Kura 4,662; na
ix.
Tarehe 3/3/2015 ambayo ndio
ilikuwa siku ya mwisho ya uandikishaji, Tume iliandikisha Wapiga Kura 2,469.
Hivyo, jumla ya Wapiga Kura wote walioandikishwa katika Kata tisa (9)
za Mji wa Makambako ni 46,709. Zoezi la Uboreshaji wa Daftari katika Kata tisa
(9) za Halmashauri ya Mji wa Makambako limefanyika kwa ufanisi na mafanikio
makubwa ambapo Tume imevuka lengo lililowekwa la Uandikishaji kwa kuandikisha
jumla ya Wapiga Kura 46,709 na kuvuka lengo
lililowekwa la kuandikisha Wapiga Kura
32,370 waliolengwa kuandikishwa kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Takwimu za
Sensa ya idadi ya Watu ya mwaka 2012.
Mashine nyingi za BVR zimeonyesha ufanisi mkubwa kwa kuwa zimekuwa
zikiandikisha idadi ya Wapiga Kura kuanzia 80 kwa siku hadi watu 160. Pamoja na
mafanikio hayo, kumekuwa na changamoto chache zilizojitokeza ikiwemo ya watu
wengi zaidi kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na
kusababisha kuwepo kwa misururu mirefu ya watu waliojitokeza katika Vituo
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Changamoto hiyo ilishughulikiwa na Tume kwa kuongeza muda wa ziada wa siku
mbili za kuandikisha Wapiga Kura baada ya muda wa siku saba za uandikishaji
kumalizika. Lengo la kuongeza siku mbili zaidi za uandikishaji lilikuwa ni kutoa fursa kwa Wapiga Kura wote ambao
walikuwa bado hawajajiandikisha kujiandikisha. Vilevile, katika kushughulikia
changamoto hizo, Tume iliongeza idadi ya BVR Kits katika baadhi ya Vituo
vilivyokuwa na idadi kubwa na misururu mirefu ya Wapiga Kura waliojitokeza
kujiandikisha. Wapiga Kura wote waliojitokeza kujiandikisha waliandikishwa pasipo
kuachwa. Kwa ujumla changamoto zote zilizojitokeza zilishughulikiwa na kupatiwa
ufumbuzi.
Tume inaendelea na Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura katika Kata nyingine za Halmashauri ya Mji wa Makambako ambapo Ratiba ya
zoezi la Uboreshaji litafanyika kama ifuatavyo:-
i.
Katika Kata ya Kitandililo
Uboreshaji umeanza kufanyika kuanzia tarehe 3/3/2015 na utamalizika tarehe
9/3/2015.
ii.
Kata ya Mahongole, Uboreshaji
utaanza kufanyika tarehe 11/3/2015 na kumalizika tarehe 17/3/2015.
iii.
Kata ya Utengule, Uboreshaji
utaanza kufanyika tarehe 09/3/2015 na kumalizika tarehe 15/3/2015.
Tume itaendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura Mkoani Njombe katika Wilaya za Njombe, Makete, Ludewa na Wanging’ombe kuanzia
tarehe 16/3/2015 hadi 12/04/2015.
Tangu zoezi hili lianze katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na
kumalizika, Wananchi wameonyesha mwamko mkubwa sana wa kujiandikisha. Ni
matumaini ya Tume kuwa Viongozi wote, Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia na
Vyombo vya Habari vitahamasisha Wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha
katika Wilaya za Njombe, Makete, Ludewa na Wangingo’mbe kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Baada ya kukamilisha Ratiba ya Uboreshaji katika Mkoa wa Njombe, Tume
itatoa Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Mikoa
mingine.
No comments:
Post a Comment